Zaburi 61 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 61:1-8

Zaburi 61

Kuomba Ulinzi

Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za uimbaji. Zaburi ya Daudi.

161:1 Za 64:1; 4:1; 86:6Ee Mungu, sikia kilio changu,

usikilize maombi yangu.

261:2 Za 6:2; 18:2; 31:2; 94:22; 1Tim 2:8Kutoka miisho ya dunia ninakuita,

ninaita huku moyo wangu unadhoofika;

uniongoze kwenye mwamba

ule ulio juu kuliko mimi.

361:3 Za 9:9; 46:1; 62:7; 59:9; Mit 18:10Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu,

ngome imara dhidi ya adui.

461:4 Kum 32:11; Mt 23:37; Ufu 3:12; Za 15:1; 23:6Natamani kukaa hemani mwako milele,

na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.

561:5 Hes 30:2; Kut 6:3; Neh 1:11; Mt 6:9; Za 56:12; 102:15; Isa 59:19; 1Kor 3:21-23; Kum 33:9Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu,

umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako.

661:6 1Fal 3:14; Za 21:4Mwongezee mfalme siku za maisha yake,

miaka yake kwa vizazi vingi.

761:7 Za 40:11; 41:12; Lk 22:69; Efe 1:20; Kol 3:1; Lk 1:32Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele;

amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde.

861:8 Kut 15:1; Hes 30:2; Kum 23:21; Za 7:17; 30:4; 56:12Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako

na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.