Zaburi 60 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 60:1-12

Zaburi 60

Kuomba Kuokolewa

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Shushani Eduthi.” Utenzi wa Daudi wa kufundisha. Wakati alipopigana na Waaramu kutoka Aramu-Naharaimu na Aramu-Soba, naye Yoabu akarudi nyuma na kuwaua Waedomu 12,000 katika Bonde la Chumvi.

160:1 2Sam 5:20; Za 18:7; 44:9; 79:5; 80:3; 60:2; 2Nya 7:14Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu,

umekasirika: sasa turejeshe upya!

2Umetetemesha nchi na kuipasua;

uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka.

360:3 Za 71:20; 75:8; Isa 29:9; 51:17; 63:6; Yer 25:16; Zek 12:2; Ufu 14:10Umewaonyesha watu wako nyakati za kukata tamaa;

umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha.

460:4 Isa 5:26; 11:10, 12; 18:3Kwa wale wanaokucha wewe,

umewainulia bendera,

ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde.

560:5 Ay 40:14; Kum 33:12; Za 108:6Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume,

ili wale uwapendao wapate kuokolewa.

660:6 Mwa 12:6; 33:17; Za 89:35; Yos 13:27Mungu amenena kutoka patakatifu pake:

“Nitaigawa Shekemu kwa ushindi

na kulipima Bonde la Sukothi.

760:7 Yos 13:31; Hes 34:19; Mwa 41:52; 49:10; Kum 33:17Gileadi ni yangu na Manase ni yangu;

Efraimu ni kofia yangu ya chuma,

nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.

860:8 2Sam 8:1Moabu ni sinia langu la kunawia,

juu ya Edomu natupa kiatu changu;

nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”

9Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome?

Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?

1060:10 Yos 7:12; Za 44:9Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi,

na hutoki tena na majeshi yetu?

1160:11 Za 146:3; Mit 3:5Tuletee msaada dhidi ya adui,

kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.

1260:12 1Nya 19:13; Ay 40:12; Za 44:5Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi,

naye atawaponda adui zetu.