Zaburi 59 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 59:1-17

Zaburi 59

Kuomba Ulinzi Wa Mungu

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Wakati Sauli alipotuma wapelelezi nyumbani mwa Daudi ili wamuue.

159:1 Za 82:259:1 Za 143:9; 20:1Ee Mungu, uniokoe na adui zangu,

unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu.

259:2 Za 14:4; 36:12; 53:4; 92:7; 94:16; 26:9; 139:19; Mit 29:10Uniponye na watu watendao mabaya,

uniokoe kutokana na wamwagao damu.

359:3 Za 56:6; 1Sam 26:18Tazama wanavyonivizia!

Watu wakali wananifanyia hila,

ingawa Ee Bwana, mimi sijakosea

wala kutenda dhambi.

459:4 Za 13:3; 119:3; Mt 5:11Sijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia.

Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya!

559:5 Za 69:6; 80:4; 84:8; 44:23; 9:5; Isa 10:3; Yer 18:23; Dan 4:35Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli!

Zinduka uyaadhibu mataifa yote,

usionyeshe huruma kwa wasaliti.

659:6 Za 22:16Hurudi wakati wa jioni,

wakibweka kama mbwa,

wakiuzurura mji.

759:7 Za 55:21; 94:4; Mit 10:32; 12:23; 15:2, 28; Ay 22:13Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao,

hutema upanga kutoka midomo yao,

nao husema, “Ni nani atakayetusikia?”

859:8 Za 2:4; 37:13; Mit 1:26Lakini wewe, Bwana, uwacheke;

unayadharau mataifa hayo yote.

959:9 Za 18:1; 9:9; 18:2; 62:2; 71:3Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe,

wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,

10Mungu wangu unipendaye.

Mungu atanitangulia,

naye atanifanya niwachekelee

wale wanaonisingizia.

1159:11 Kum 4:9; 6:12; Za 3:3; 84:9; 89:10; 106:27; 144:6; Isa 33:3; Mwa 4:12, 13Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu,

au sivyo watu wangu watasahau.

Katika uwezo wako wafanye watangetange

na uwashushe chini.

1259:12 Za 10:7; 64:8; Mit 10:14; 12:13; Isa 2:12; 5:15; Sef 3:11Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao,

kwa ajili ya maneno ya midomo yao,

waache wanaswe katika kiburi chao.

Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka,

1359:13 Za 83:18; 104:35wateketeze katika ghadhabu,

wateketeze hadi wasiwepo tena.

Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia

kwamba Mungu anatawala juu ya Yakobo.

14Hurudi jioni,

wakibweka kama mbwa,

wakiuzurura mji.

1559:15 Ay 15:23Wanatangatanga wakitafuta chakula,

wasipotosheka hubweka kama mbwa.

1659:16 Za 5:3; 88:13; 101:1; 108:1; 1Sam 2:10; 2Sam 22:3; Kum 4:30Lakini mimi nitaziimba nguvu zako,

asubuhi nitaimba juu ya upendo wako;

kwa maana wewe ndiwe ngome yangu

na kimbilio langu wakati wa shida.

1759:17 Za 59:1Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa.

Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,

Mungu unipendaye.