Zaburi 57
Kuomba Msaada
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Baada ya kumponyoka Sauli pangoni.
157:1 Isa 26:20Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie,
kwa maana nafsi yangu inakukimbilia.
Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia
mpaka maafa yapite.
257:2 Za 138:8Namlilia Mungu Aliye Juu Sana,
Mungu atimizaye makusudi yake kwangu.
357:3 Za 18:9, 16; 69:14; 142:5, 7; 56:1; 25:10; 40:11; 115:1Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa,
akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali;
Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake.
457:4 Za 35:17; 55:21; 64:3; Mit 30:14Niko katikati ya simba,
nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu:
watu ambao meno yao ni mikuki na mishale,
ambao ndimi zao ni panga kali.
557:5 Za 108:5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
utukufu wako na uenee duniani kote.
657:6 Es 6:13; Za 31:4; 9:15; 140:5; 7:15; 38:6; 10:9; 145:14; Mit 28:10; Mhu 10:8Waliitegea miguu yangu nyavu,
nikainamishwa chini na dhiki.
Wamechimba shimo katika njia yangu,
lakini wametumbukia humo wao wenyewe.
757:7 Za 112:7; 108:1Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti;
nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.
857:8 Za 33:2; 149:3; 150:3; Amu 5:12Amka, nafsi yangu!
Amka, kinubi na zeze!
Nitayaamsha mapambazuko.
9Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa;
nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.
1057:10 Za 36:5; 108:4Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni,
uaminifu wako unazifikia anga.
1157:11 Za 8:1; 149:3; 150:3; Amu 5:12Ee Mungu, utukuzwe juu mbinguni,
utukufu wako na uwe duniani pote.