Zaburi 56 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 56:1-13

Zaburi 56

Kumtumaini Mungu

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Njiwa mkimya wa mbali.” Utenzi wa Daudi. Baada ya kukamatwa na Wafilisti huko Gathi.

156:1 Za 6:2; 57:1-3; 17:9; 31:9Ee Mungu unihurumie, maana watu wananifuatia vikali;

mchana kutwa wanazidisha mashambulizi yao.

256:2 Za 57:3; 35:1, 25; 124:3Wasingiziaji wangu wananifuatia mchana kutwa,

wengi wananishambulia kwa kiburi chao.

356:3 1Sam 30:6; 2Nya 20:3; Za 55:4-5, 23Wakati ninapoogopa,

nitakutumaini wewe.

456:4 Ebr 13:5, 6; 13:6; Za 27:1; 118:6; Mt 10:28Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu,

katika Mungu ninatumaini; sitaogopa.

Mwanadamu apatikanaye na kufa,

atanitenda nini?

556:5 Za 41:7; 2Pet 3:16Mchana kutwa wanayageuza maneno yangu,

siku zote wanapanga shauri la kunidhuru.

656:6 Mk 3:6; Za 59:3; 94:21; 71:16; 17:11; Mdo 4:27, 28Wananifanyia hila, wanajificha,

wanatazama hatua zangu,

wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu.

756:7 Mt 19:5; Eze 17:15; Rum 2:3; Ebr 12:25; Za 36:12; 55:23Wasiepuke kwa vyovyote,

Ee Mungu, katika hasira yako yaangushe mataifa.

856:8 2Fal 20:5; Isa 4:3; Dan 7:10; 12:1; Mal 3:16Andika maombolezo yangu,

orodhesha machozi yangu katika gombo lako:

je, haya hayapo katika kumbukumbu zako?

956:9 Rum 8:31; Za 9:3; 102:2; Hes 14:8; Kum 31:6Ndipo adui zangu watarudi nyuma

ninapoita msaada.

Kwa hili nitajua kwamba Mungu

yuko upande wangu.

10Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu,

katika Bwana, ambaye neno lake ninalisifu,

11katika Mungu ninatumaini, sitaogopa.

Mwanadamu anaweza kunitenda nini?

1256:12 Za 50:14; 116:14-16Ee Mungu, nina nadhiri kwako,

nitakutolea wewe sadaka zangu za shukrani.

1356:13 Za 30:3; 33:19; 49:15; 86:13; 107:20; 116:8; Ay 33:30Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti

na miguu yangu kwenye kujikwaa,

ili niweze kuenenda mbele za Mungu

katika nuru ya uzima.