Zaburi 55 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 55:1-23

Zaburi 55

Maombi Ya Mtu Aliyesalitiwa Na Rafiki

Kwa mwimbishaji. Na ala za uimbaji. Utenzi wa Daudi.

155:1 Za 27:9; Mao 3:56Ee Mungu, sikiliza maombi yangu,

wala usidharau hoja yangu.

255:2 1Sam 1:15-16; Za 4:1; 77:3; 86:6-7; 142:2Nisikie na unijibu.

Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa

355:3 2Sam 16:6-8; 17:9; Za 143:3; 44:16; 71:11kwa sauti ya adui,

kwa kukaziwa macho na waovu,

kwa sababu wananiletea mateso juu yangu

na kunitukana kwa hasira zao.

455:4 Ay 18:11; Za 6:3; 102:3-5; Yn 12:27; Mt 26:37, 38; 2Kor 1:8-10Moyo wangu umejaa uchungu,

hofu ya kifo imenishambulia.

555:5 Ay 4:14; Eze 7:18; 2Kor 7:15; Isa 21:4; Kum 28:67; Yer 46:5; 49:5Woga na kutetemeka vimenizunguka,

hofu kuu imenigharikisha.

6Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa!

Ningeruka niende mbali kupumzika.

755:7 1Sam 23:14Ningalitorokea mbali sana

na kukaa jangwani,

855:8 Za 31:20; 77:18; Isa 4:6; 25:4; 28:2; 29:6; 32:2ningaliharakisha kwenda mahali pa salama,

mbali na tufani kali na dhoruba.”

955:9 Mwa 4:17; 11:9; Mdo 2:4; Za 11:5; Isa 59:6; Yer 6:7; Eze 7:11; Hab 1:3Ee Bwana, uwatahayarishe waovu

na uwachanganyishie semi zao,

maana nimeona jeuri na ugomvi mjini.

1055:10 1Pet 5:8Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake,

uovu na dhuluma vimo ndani yake.

1155:11 Za 5:9; 10:7Nguvu za uharibifu zinatenda kazi mjini,

vitisho na uongo haviondoki mitaani mwake.

12Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia,

kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu,

ningejificha asinione.

1355:13 2Sam 15:12Kumbe ni wewe, mwenzangu,

mshiriki na rafiki yangu wa karibu,

1455:14 Mdo 1:16-17; Za 42:4ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri,

tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu.

1555:15 Za 64:7; 49:14; Mit 6:5; Isa 29:5; 47:9, 11; 1The 5:3; Hes 16:30Kifo na kiwajie adui zangu ghafula,

na washuke kuzimu wangali hai,

kwa maana uovu upo ndani yao.

16Lakini ninamwita Mungu,

naye Bwana huniokoa.

1755:17 Za 141:2; 88:13; 92:2; 5:3; Mdo 3:1; 10:9; 10:3, 30; Lk 18:1; Dan 6:10Jioni, asubuhi na adhuhuri

ninalia kwa huzuni,

naye husikia sauti yangu.

1855:18 2Nya 32:7Huniokoa nikawa salama katika vita

vilivyopangwa dhidi yangu,

ingawa watu wengi hunipinga.

1955:19 Kum 33:27; Za 29:10; 78:59; 36:1; 64:4; Kut 15:18Mungu anayemiliki milele,

atawasikia na kuwaadhibu,

watu ambao hawabadilishi njia zao,

wala hawana hofu ya Mungu.

2055:20 Za 7:4; 41:9Mwenzangu hushambulia rafiki zake,

naye huvunja agano lake.

2155:21 Za 59:7; 57:4; 12:2; 64:3; Ufu 1:16; Mit 5:3; 6:24; 12:18Mazungumzo yake ni laini kama siagi,

hata hivyo vita vimo moyoni mwake.

Maneno yake ni mororo kuliko mafuta,

hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa.

2255:22 1Pet 5:7; Za 15:5; 18:35; 112:6; 21:7; 37:24; Mt 6:25-34Mtwike Bwana fadhaa zako,

naye atakutegemeza,

hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.

2355:23 Za 5:6; 11:1; 9:15; 73:18; 94:13; 25:2; 30:3; 56:3; Isa 14:15; Eze 28:8; Lk 8:31; Ay 15:32Lakini wewe, Ee Mungu,

utawashusha waovu katika shimo la uharibifu.

Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila,

hawataishi nusu ya siku zao.

Lakini mimi ninakutumaini wewe.