Zaburi 53 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 53:1-6

Zaburi 53

Uovu Wa Wanadamu

(Zaburi 14)

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi. Utenzi wa Daudi.

153:1 Za 107:17; 74:22; 10:4; Mit 10:23; Rum 3:10Mpumbavu anasema moyoni mwake,

“Hakuna Mungu.”

Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa,

hakuna hata mmoja atendaye mema.

253:2 Za 33:13; 82:5; Yer 4:22; 8:8; 2Nya 15:2Mungu anawachungulia wanadamu chini

kutoka mbinguni

aone kama wako wenye akili,

wowote wanaomtafuta Mungu.

353:3 Rum 3:10-12; Mhu 7:29Kila mmoja amegeukia mbali,

wameharibika wote pamoja,

hakuna atendaye mema.

Naam, hakuna hata mmoja!

453:4 Yer 4:22Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza:

wale ambao huwala watu wangu

kama watu walavyo mkate,

hao ambao hawamwiti Mungu?

553:5 Law 26:17; Eze 6:5; 2Fal 17:20; 23:14; Za 141:7; Mao 5:22; Yer 6:30; 14:19; 8:1; Ay 8:22Hapo waliingiwa na hofu kuu,

ambapo hapakuwa cha kutetemesha.

Mungu alitawanya mifupa ya wale waliokushambulia;

uliwaaibisha, kwa sababu Mungu aliwadharau.

6Laiti wokovu wa Israeli ungalikuja kutoka Sayuni!

Wakati Mungu arejeshapo wafungwa wa watu wake,

Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi!