Zaburi 52 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 52:1-9

Zaburi 52

Hukumu Ya Mungu

Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi. Baada ya Doegi, Mwedomu kumwendea Sauli na kumjulisha kuwa: “Daudi amekwenda nyumbani kwa Ahimeleki.”

152:1 Za 10:3; 44:8; 94:4; 1Sam 21:7Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya?

Kwa nini unajivuna mchana kutwa,

wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu?

252:2 Za 5:9; 59:7; Hes 6:5; Mit 12:18Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi.

Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila.

352:3 Kut 10:10; Za 58:3; 1Sam 12:25; Amo 5:14, 15; Yn 3:20; Ufu 21:8; Yer 9:4, 5Unapenda mabaya kuliko mema,

uongo kuliko kusema kweli.

452:4 Za 5:9; 10:7; 109:2; 120:2, 3; Mit 10:31; 12:19Unapenda kila neno lenye kudhuru,

ewe ulimi wenye hila!

552:5 Kum 28:63; 29:28; Ay 28:13; 40:12; Isa 22:19; Mit 2:22; Eze 17:24Hakika Mungu atakushusha chini

kwa maangamizi ya milele:

atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu

kutoka hema yako,

atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai.

652:6 Ay 22:19; Za 58:10Wenye haki wataona na kuogopa,

watamcheka, wakisema,

752:7 2Sam 22:3; Za 49:6; Mk 10:23; Mit 11:28; Ay 31:24, 25“Huyu ni yule mtu ambaye

hakumfanya Mungu kuwa ngome yake,

bali alitumainia wingi wa utajiri wake,

na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”

Neema Ya Mungu

852:8 Ufu 11:4; Za 1:3; 6:4; 13:5; 54:6Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni

unaostawi katika nyumba ya Mungu,

nautegemea upendo wa Mungu usiokoma

milele na milele.

952:9 Ay 7:6; Za 16:3; 30:12; 25:3; 54:6; Kum 7:6Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda,

nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema.

Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.