Zaburi 5 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 5:1-12

Zaburi 5

Sala Kwa Ajili Ya Ulinzi Wakati Wa Hatari

Kwa mwimbishaji. Kwa filimbi. Zaburi ya Daudi.

15:1 1Fal 8:29; Za 17:1; 38:9; 40:1; 116:2; Dan 9:18; Isa 35:10; 51:11Ee Bwana, tegea sikio maneno yangu,

uangalie kupiga kite kwangu.

25:2 Ay 19:7; 24:12; 36:5; Za 44:4; 68:24; 84:3Sikiliza kilio changu ili unisaidie,

Mfalme wangu na Mungu wangu,

kwa maana kwako ninaomba.

35:3 Isa 28:19; 50:4; Yer 21:12; Sef 3:5; Eze 46:13; Hab 2:1; Rum 8:19; Za 30:5; 62:1; 119:81; 130:5Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana;

asubuhi naleta haja zangu mbele zako,

na kusubiri kwa matumaini.

45:4 Za 1:5; 11:5; 104:35; Mit 2:22; Mal 2:17Wewe si Mungu unayefurahia uovu,

kwako mtu mwovu hataishi.

55:5 2Fal 19:32; Za 1:5; 45:10; 1:3; 119:104; 73:3; 75:4; 14:1; Isa 33:19; 37:33; Mit 8:13; Hab 1:13Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako,

unawachukia wote watendao mabaya.

65:6 Mit 19:22; Yn 8:44; Mdo 5:3; Ufu 21:8Unawaangamiza wasemao uongo.

Bwana huwachukia

wamwagao damu na wadanganyifu.

75:7 Kum 13:4; Yer 44:10; Dan 6:26; 2Sam 12:16; Za 138:2; 1Fal 8:48Lakini mimi, kwa rehema zako kuu,

nitakuja katika nyumba yako,

kwa unyenyekevu, nitasujudu

kuelekea Hekalu lako takatifu.

85:8 Za 23:3; 31:1; 71:2; 85:13; 89:16; Mit 8:20; 1Fal 8:36; Yn 1:23Niongoze katika haki yako, Ee Bwana,

kwa sababu ya adui zangu,

nyoosha njia yako mbele yangu.

95:9 Yer 5:16; Lk 11:44; Za 12:2; 28:3; 36:3; Yer 9:8; Rum 3:135:9 Isa 13:8; Yer 46:5Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika,

mioyo yao imejaa maangamizi.

Koo lao ni kaburi lililo wazi,

kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu.

105:10 Mao 1:5; 3:42; Za 78:40; 106:7; 107:11Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu!

Hila zao ziwe anguko lao wenyewe.

Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi,

kwa kuwa wamekuasi wewe.

115:11 1Kor 2:9; Za 33:1; 81:1; 90:14; 92:4; 95:1; 145:7; 69:36; 119:132; Ay 22:19Lakini wote wakimbiliao kwako na wafurahi,

waimbe kwa shangwe daima.

Ueneze ulinzi wako juu yao,

ili wale wapendao jina lako

wapate kukushangilia.

125:12 Za 112:2; 32:7; Mwa 15:1Kwa hakika, Ee Bwana, unawabariki wenye haki,

unawazunguka kwa wema wako kama ngao.