Zaburi 49 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 49:1-20

Zaburi 49

Upumbavu Wa Kutegemea Mali

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.

149:1 Isa 1:2; Za 33:8; 78:1Sikieni haya, enyi mataifa yote,

sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii.

249:2 Za 62:9Wakubwa kwa wadogo,

matajiri na maskini pamoja:

349:3 Za 37:30; 119:130Kinywa changu kitasema maneno ya hekima,

usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu.

449:4 Za 33:2; 78:2; 1Sam 16:16; Mit 1:6; Eze 12:22; 16:44; 18:2, 3; Hes 12:8; Lk 4:23Nitatega sikio langu nisikilize mithali,

nitafafanua kitendawili kwa zeze:

549:5 Za 23:4; 27:1Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja,

wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka,

649:6 Yer 48:7; Za 10:3; 73:12; Ay 22:25; 36:19wale wanaotegemea mali zao

na kujivunia utajiri wao mwingi?

749:7 Mt 16:26Hakuna mwanadamu awaye yote

awezaye kuukomboa uhai wa mwingine,

au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake.

849:8 Hes 35:31; Mt 16:26; Ay 36:18Fidia ya uhai ni gharama kubwa,

hakuna malipo yoyote yanayotosha,

949:9 Za 22:29; 89:48; 16:10; Ebr 9:27ili kwamba aishi milele

na asione uharibifu.

1049:10 Mhu 2:16, 18, 21; Za 92:6; 94:8; Ay 27:17; Lk 12:20Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa;

wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia

na kuwaachia wengine mali zao.

1149:11 Mk 5:3; Lk 8:27; Za 106:31; Kum 3:14Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele,

makao yao vizazi vyote;

ingawa walikuwa na mashamba

na kuyaita kwa majina yao.

1249:12 Ay 14:2Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu;

anafanana na mnyama aangamiaye.

1349:13 Lk 12:20Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe,

pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao.

1449:14 Yer 43:11; Isa 14:2; Hes 16:30; Eze 31:14; Mal 4:3; Ay 21:13; Ufu 2:26; 1Kor 6:2; Za 9:17; 55:15; Dan 7:18, 22; Lk 22:30; 2Tim 2:12Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini,49:14 Kaburini hapa ina maana ya Sheol kwa Kiebrania, yaani Kuzimu.

nacho kifo kitawala.

Wanyofu watawatawala asubuhi,

maumbile yao yataozea kaburini,

mbali na majumba yao makubwa ya fahari.

1549:15 Za 56:13; Hos 13:14; Mwa 5:24Lakini Mungu atakomboa uhai49:15 Au: nafsi. wangu na kaburi,

hakika atanichukua kwake.

16Usitishwe mtu anapotajirika,

fahari ya nyumba yake inapoongezeka,

1749:17 1Tim 6:7; Za 17:14kwa maana hatachukua chochote atakapokufa,

fahari yake haitashuka pamoja naye.

1849:18 Za 10:6; Lk 12:19Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri,

na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa,

1949:19 Mwa 15:15; Ay 33:30atajiunga na kizazi cha baba zake,

ambao hawataona kamwe nuru ya uzima.

2049:20 Mit 16:16; Mhu 3:19-21Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu

ni kama wanyama waangamiao.