Zaburi 47 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 47:1-9

Zaburi 47

Mtawala Mwenye Enzi Yote

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.

147:1 2Fal 11:12; Za 33:3Pigeni makofi, enyi mataifa yote,

mpigieni Mungu kelele za shangwe!

247:2 Kum 7:21; Mal 1:14; Mwa 14:18; Neh 1:5; Za 2; 6; 48:2; 95:3; Mt 5:35Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana,

Mfalme mkuu juu ya dunia yote!

347:3 Za 18:39, 47; Isa 14:6Ametiisha mataifa chini yetu

watu wengi chini ya miguu yetu.

447:4 Za 2:8; 16:6; 78:55; 1Pet 1:4; Amo 6:8; 8:7Alituchagulia urithi wetu,

fahari ya Yakobo, aliyempenda.

547:5 Za 68:18; Efe 4:8Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,

Bwana kwa sauti za tarumbeta.

647:6 2Sam 22:50Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa,

mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.

747:7 Zek 14:9, 19; 1Nya 16:7; Kol 3:16; 1Kor 14:15Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote,

mwimbieni zaburi za sifa.

847:8 1Nya 16:31; 1Fal 22:19; Za 9:4; Ufu 4:9Mungu anatawala juu ya mataifa,

Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.

947:9 Ay 25:2; Za 46:10; 97:9Wakuu wa mataifa wanakusanyika

kama watu wa Mungu wa Abrahamu,

kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu;

yeye ametukuka sana.