Zaburi 45 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 45:1-17

Zaburi 45

Wimbo Wa Arusi Ya Kifalme

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Yungiyungi.” Utenzi wa wana wa Kora. Wimbo wa arusi.

1Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema

ninapomsimulia mfalme mabeti yangu;

ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi.

245:2 Lk 4:22; Za 21:6Wewe ni bora kuliko watu wengine wote

na midomo yako imepakwa neema,

kwa kuwa Mungu amekubariki milele.

345:3 Kum 32:41; Ufu 1:16; Za 21:5; 149:6; 2Sam 1:19; Ay 40:10Jifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu,

jivike fahari na utukufu.

445:4 Ufu 6:2; Sef 2:3; Za 21:8; 65:5; 66:3; Kum 4:34Katika fahari yako, songa mbele kwa ushindi,

kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki,

mkono wako wa kuume na uonyeshe matendo ya kutisha.

545:5 Kum 32:23; Hes 24:8; Isa 50:10; Za 56:3, 11; 9:13; 92:9; Mao 3:24Mishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme,

mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako.

645:6 Mwa 21:33; Mao 5:13; Za 93:2; Isa 9:6, 7; Ebr 1:8Ee Mungu, kiti chako cha enzi

kitadumu milele na milele,

fimbo ya utawala wa haki

itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako.

745:7 Za 33:5; 11:5; 2:2; 23:5; Ebr 1:9; Eze 7:26; Isa 45:1; 61:1; Yn 20:17; Mt 3:15; Zek 4:14Unaipenda haki na kuchukia uovu;

kwa hiyo Mungu, Mungu wako,

amekuweka juu ya wenzako,

kwa kukupaka mafuta ya furaha.

845:8 Kum 28:8; Wim 1:3; 4:10; Mwa 37:25; Hes 24:6; Yn 19:39; Kut 30:24; 1Fal 22:39; Za 144:9; 150:4; Isa 38:20; Mt 27:9Mavazi yako yote yana harufu nzuri

ya manemane, udi na mdalasini;

kutoka kwenye majumba ya kifalme

yaliyopambwa kwa pembe za ndovu,

sauti za vinanda vya nyuzi

zinakufanya ufurahi.

945:9 Wim 6:8; Isa 62:5; Mwa 10:29; 1Fal 2:19Binti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa;

kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri.

1045:10 Yer 5:1; Rut 1:11; 1:16; Kum 21:13Sikiliza, ewe binti, fikiri na utege sikio:

Sahau watu wako na nyumba ya baba yako.

1145:11 Mao 2:15; Efe 5:33; Isa 54:5; Za 95:6; Es 1:11Mfalme ameshangazwa na uzuri wako;

mheshimu, kwa kuwa yeye ni bwana wako.

1245:12 Yos 19:29; 1Fal 9:16; 2Nya 9:24Binti wa Tiro atakuletea zawadi,

watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako.

1345:13 Isa 61:10; Kut 39:3; Ufu 19:7, 8Utukufu wote una binti mfalme katika chumba chake;

vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu.

1445:14 Amu 5:30; Es 2:15; Wim 1:3Anaongozwa kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa,

mabikira wenzake wanamfuata

na wanaletwa kwako.

1545:15 Es 8:17Wanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha,

na kuingia katika jumba la mfalme.

1645:16 1Sam 2:8; Za 68:27; 113:8; 1Pet 2:9; Ufu 1:6Wana wenu watachukua nafasi za baba zenu,

mtawafanya wakuu katika nchi yote.

1745:17 Isa 11:10; Mal 1:11; Kut 3:15; Ufu 22:5; Za 33:11; 138:4; 119:90; 135:13Nitadumisha kumbukumbu lako katika vizazi vyote,

kwa hiyo mataifa watakusifu milele na milele.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

詩篇 45:1-17

第45篇

婚禮詩歌

可拉後裔作的訓誨詩,也是情歌,交給樂長,調用「百合花」。

1我心中湧出美麗的詩章,

我要把它獻給王,

我的舌頭是詩人手上的妙筆。

2你俊美無比,口出恩言,

因此上帝永遠賜福給你。

3英勇的王啊,

佩上你的寶劍,

展示你的尊貴和威嚴!

4你威嚴無比,所向披靡,

捍衛真理、謙卑和公義。

願你的右手彰顯可畏的作為!

5你的利箭刺穿敵人的心窩,

列國臣服在你腳下。

6上帝啊,你的寶座永遠長存,

你以公義的杖執掌王權。

7你喜愛公義,憎惡邪惡,

所以上帝,你的上帝,

用喜樂之油膏你,

使你超過同伴。

8你的衣袍散發出沒藥、沉香和肉桂的芬芳,

你陶醉在象牙宮的弦樂中。

9眾公主在你的貴客中,

俄斐金飾的王后站在你右邊。

10女子啊,要聆聽,

要側耳傾聽:不要再掛念家鄉的父老,

11王就會喜歡你的美貌,

你要敬重他,因他是你的主。

12泰爾人必來送禮,

富人必來取悅你。

13公主身穿金線衣,無比華貴。

14她身披錦繡,

由侍女伴隨前來見王,

15她們歡喜快樂地被帶入王宮。

16你的子孫將來要繼承祖先的王位,

你要立他們在各地做王。

17我要使萬代銘記你的名,

列邦必永遠稱謝你。