Zaburi 44 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 44:1-26

Zaburi 44

Kuomba Ulinzi Wa Mungu

Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora.

144:1 2Sam 7:22; 1Nya 17:20; Yer 26:11; Amu 6:13; Kum 32:7; Ay 37:23Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu,

baba zetu wametueleza

yale uliyotenda katika siku zao,

siku za kale.

244:2 Kut 15:17; Kum 7:1; Yos 10:42; 3:10; Mdo 7:45; Isa 60:21; Amu 4:23; 2Nya 14:13; Za 80:9; Yer 32:23Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa

na ukawapanda baba zetu,

uliangamiza mataifa

na kuwastawisha baba zetu.

344:3 Yos 24:12; Kut 15:16; Za 78:54; 77:15; 79:11; 89:10, 15; Isa 40:10; 52:10; 63:5; Kum 4:37Sio kwa upanga wao waliipata nchi,

wala si mkono wao uliwapatia ushindi;

ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume,

na nuru ya uso wako,

kwa kuwa uliwapenda.

444:4 Za 24:7; 5:2; 21:5; 74:12Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu,

unayeamuru ushindi kwa Yakobo.

544:5 Yos 23:5; Za 60:12; 108:13; Dan 8:10Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu;

kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu.

644:6 Za 33:16; Hos 1:7; Mwa 48:22Siutumaini upinde wangu,

upanga wangu hauniletei ushindi;

744:7 Kum 20:4; Ay 8:2bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu,

unawaaibisha watesi wetu.

844:8 1Kor 1:3; Rum 2:17; Za 34:2; 52:1; 30:12; 2Kor 10:17Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa,

nasi tutalisifu jina lako milele.

944:9 Kum 8:3; 31:17; Za 43:2; 107:39; 108:11; Isa 5:15; Yos 7:12Lakini sasa umetukataa na kutudhili,

wala huendi tena na jeshi letu.

1044:10 Law 26:17; Amu 2:14; Kum 28:25Umetufanya turudi nyuma mbele ya adui,

nao watesi wetu wametuteka nyara.

1144:11 Yer 12:3; 32:37; Law 26:33; Zek 2:6; Kum 4:27; Eze 6:8; Lk 21:24; Za 9:11; 60:1; 2Fal 17:6Umetuacha tutafunwe kama kondoo

na umetutawanya katika mataifa.

1244:12 Kum 32:30; Isa 50:1; 52:3; Yer 15:13Umewauza watu wako kwa fedha kidogo,

wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao.

1344:13 2Nya 29:8; Isa 30:3; Yer 25:9; 42:18; 44:8; Kum 28:37; Mik 2:6; Za 79:4; 80:6; 89:41; Eze 23:32Umetufanya lawama kwa jirani zetu,

dharau na dhihaka kwa wale wanaotuzunguka.

1444:14 1Fal 9:7; 2Fal 19:21Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa,

mataifa hutikisa vichwa vyao.

1544:15 Mwa 30:23; 2Nya 32:21; Za 35:26; 34:5Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa,

na uso wangu umejaa aibu tele,

1644:16 Za 42:10; 10:13; 55:3; 74:10; 1Sam 18:25; Yer 11:19; Rum 12:19kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana,

kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi.

1744:17 Kum 6:12; 32:18; Mit 3:1; Dan 9:13; Za 119:16, 61, 153, 176Hayo yote yametutokea,

ingawa tulikuwa hatujakusahau

wala hatujaenda kinyume na agano lako.

1844:18 Za 119:51, 157Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma;

nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako.

1944:19 2Nya 14:13; Za 51:8; Isa 43:12; Ay 30:29; 3:5Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha,

na ukatufunika kwa giza nene.

2044:20 Kum 32:18; Amu 4:7; Isa 43:12; Kut 20:3; Yer 5:12Kama tungalikuwa tumelisahau jina la Mungu wetu

au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni,

2144:21 1Sam 16:7; 1Fal 8:39; Yn 2:25; Mit 15:11; Yer 12:3; 17:10; Ay 31:14; Za 139:1; Mhu 12:14; Mdo 1:24; Ufu 2:23; Rum 2:16; Ebr 4:12je, Mungu hangaligundua hili,

kwa kuwa anazijua siri za moyo?

2244:22 Yer 11:19; 12:3; Isa 53:7; Rum 8:36Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa;

tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.

2344:23 Za 7:6; 78:65; 59:5; 74:1; 77:7Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala?

Zinduka! Usitukatae milele.

2444:24 Mao 5:20Kwa nini unauficha uso wako

na kusahau taabu na mateso yetu?

2544:25 Za 119:25Tumeshushwa hadi mavumbini,

miili yetu imegandamana na ardhi.

2644:26 Za 102:13; 26:11; 12:5; 6:4; Hes 10:25Inuka na utusaidie,

utukomboe kwa sababu ya upendo wako usio na mwisho.