KITABU CHA PILI
(Zaburi 42–72)
Zaburi 42
Maombi Ya Mtu Aliye Uhamishoni
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora.
142:1 Ay 19:27; Yoe 1:20; Za 18:33; 119:131; Kum 10:7Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji,
ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu.
242:2 Za 43:4; 143:6; 84:7; 63:1; Yos 3:10; 1The 1:9; Yn 7:37; Rum 9:26; 1Sam 14:19; Mt 16:16; 9:26Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai.
Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu?
342:3 Ay 3:24; Mik 7:10; Za 79:10; 115:2; Yoe 2:17Machozi yangu yamekuwa chakula changu
usiku na mchana,
huku watu wakiniambia mchana kutwa,
“Yuko wapi Mungu wako?”
442:4 1Sam 1:15; Isa 2:2; 30:29; Yon 2:9; Ezr 3:13; Yos 6:5; Za 35:18; 109:30; 55:14; 122:1; 95:2; 100:4; 147:7Mambo haya nayakumbuka
ninapoimimina nafsi yangu:
Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu,
nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu,
kwa kelele za shangwe na za shukrani
katikati ya umati uliosherehekea.
542:5 Mao 3:20; Mt 26:38; Za 9:1; 38:6; 77:3; 25:5; 71:14; 56:3, 11; 18:46; Ay 20:2; Isa 50:10Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?
Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?
Weka tumaini lako kwa Mungu,
kwa sababu bado nitamsifu,
Mwokozi wangu na 642:6 Za 43:5; 63:6; 7:11; Mwa 13:10; Hes 13:29; Kum 3:8; 4:48Mungu wangu.
Nafsi yangu inasononeka ndani yangu;
kwa hiyo nitakukumbuka
kutoka nchi ya Yordani,
katika vilele vya Hermoni,
kutoka Mlima Mizari.
742:7 Eze 7:26; Mwa 1:2; 7:11; Za 69:2; Yon 2:3Kilindi huita kilindi,
katika ngurumo za maporomoko ya maji yako;
mawimbi yako yote pamoja na viwimbi
vimepita juu yangu.
842:8 Za 57:3; 16:7; 133:3; Mhu 5:18; 8:15; Kum 28:8Mchana Bwana huelekeza upendo wake,
usiku wimbo wake uko nami:
maombi kwa Mungu wa uzima wangu.
942:9 Za 18:31; 10:11; 35:14; 106:42; 9:13; 43:2; Ay 20:19Ninamwambia Mungu Mwamba wangu,
“Kwa nini umenisahau?
Kwa nini niendelee kuomboleza,
nikiwa nimeonewa na adui?”
1042:10 Za 89:51; 119:42; 44:16; 6:2; 102:8; Kum 32:27Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makali
adui zangu wanaponidhihaki,
wakiniambia mchana kutwa,
“Yuko wapi Mungu wako?”
1142:11 Za 43:5Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?
Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?
Weka tumaini lako kwa Mungu,
kwa sababu bado nitamsifu,
Mwokozi wangu na Mungu wangu.
卷二:詩篇42—72
第42篇
流落異鄉者的禱告
可拉後裔作的訓誨詩,交給樂長。
1上帝啊,我的心切慕你,
像鹿切慕溪水。
2我心裡渴慕上帝,
渴慕永活的上帝,
我何時才能去朝見祂呢?
3我晝夜以淚為食,
人們整天譏笑我:
「你的上帝在哪裡?」
4從前我與眾人同行,帶領大家去上帝的殿,
在歡呼、感恩聲中一起過節。
我回想這些事,
心中無限憂傷。
5我的心啊!
你為何沮喪?為何在我裡面煩躁?
要仰望上帝,
因為我還要讚美祂——我的救主,我的上帝。
6我的上帝啊,我心中沮喪,
便在約旦之地、黑門山和米薩山想起你。
7你的瀑布發出巨響,
迴盪在深淵之間,
你的洪濤巨浪淹沒我。
8白天耶和華將祂的慈愛澆灌我;
夜間我歌頌祂,
向賜我生命的上帝禱告。
9我對我的磐石上帝說:
「你為何忘記我?
為何要我受仇敵的攻擊,使我哀傷不已呢?」
10仇敵的辱罵刺骨鑽心。
他們整天對我說:
「你的上帝在哪裡?」
11我的心啊!
你為何沮喪?為何在我裡面煩躁?
要仰望上帝,
因為我還要讚美祂——我的救主,我的上帝。