Zaburi 41 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 41:1-13

Zaburi 41

Maombi Ya Mtu Mgonjwa

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

141:1 Kum 14:29; Ay 24:4; Za 25:17; Mit 14:21; Mk 10:21Heri mtu yule anayemjali mnyonge,

Bwana atamwokoa wakati wa shida.

241:2 Za 12:5; 32:7; 71:20; 119:88, 159; 138:7; 143:1; 37:22; Ezr 9:9; Kum 6:24Bwana atamlinda na kuyahifadhi maisha yake,

atambariki katika nchi

na hatamwacha katika tamaa ya adui zake.

341:3 Za 6:6; 2Fal 1:4; 2Sam 13:5Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani,

atamwinua kutoka kitandani mwake.

441:4 Za 6:2; 9:13; Kum 32:39; Za 51:4Nilisema, “Ee Bwana nihurumie,

niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.”

541:5 Za 38:12Adui zangu wanasema kwa hila,

“Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.”

641:6 Za 12:2; 101:7; Mt 5:11; Mit 26:24; Law 19:16Kila anapokuja mtu kunitazama,

huzungumza uongo,

huku moyo wake hukusanya masingizio;

kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko.

741:7 Za 71:10Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu,

hao huniwazia mabaya sana, wakisema,

841:8 2Fal 1:4“Ugonjwa mbaya sana umempata,

kamwe hatainuka tena kitandani mwake.”

941:9 Oba 1:7; Yn 13:18; 2Sam 15:12; Ay 19:14, 19; Hes 30:2; Lk 22:21; Za 55:20; 89:34; Mt 26:23Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini,

yule aliyekula chakula changu

ameniinulia kisigino chake.

1041:10 Za 3:3; 9:13; 2Sam 3:39Lakini wewe, Ee Bwana, nihurumie,

ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi.

1141:11 Hes 14:8; Za 25:2Najua kwamba wapendezwa nami,

kwa kuwa adui yangu hanishindi.

1241:12 Za 21:6; 61:7; 34:15; 25:21; 18:35; 37:17; 63:8; Ay 4:7; Mdo 2:38Katika uadilifu wangu unanitegemeza

na kuniweka kwenye uwepo wako milele.

1341:13 Mwa 24:27; Za 72:18, 19; 89:52; 106:48Msifuni Bwana, Mungu wa Israeli,

tangu milele na hata milele.

Amen na Amen.