Zaburi 40 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 40:1-17

Zaburi 40

Wimbo Wa Sifa

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

140:1 Za 37:7; 116:1; 6:9; 31:22; 34:15; 7:15; 145:19Nilimngoja Bwana kwa saburi,

naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

240:2 Ay 9:31; 30:19; Za 7:15; 69:14; 31:8; 27:5Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu,

kutoka matope na utelezi;

akaiweka miguu yangu juu ya mwamba

na kunipa mahali imara pa kusimama.

340:3 Za 28:7; 52:6; 64:9; Ufu 5:9; Kut 14:31Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu,

wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.

Wengi wataona na kuogopa

na kuweka tumaini lao kwa Bwana.

440:4 Za 2:12; 34:8; 84:12; 101:5; 4:2; 138:6; Kum 31:20; Mit 3:34; 16:5; Isa 65:5; 1Pet 5:5Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake,

asiyewategemea wenye kiburi,

wale wenye kugeukia miungu ya uongo.

540:5 Kum 4:34; Isa 55:8; Za 75:1; 105:5; 136:4; 139:18; 71:15; 139:15Ee Bwana Mungu wangu,

umefanya mambo mengi ya ajabu.

Mambo uliyopanga kwa ajili yetu

hakuna awezaye kukuhesabia;

kama ningesema na kuyaelezea,

yangekuwa mengi mno kuyaelezea.

640:6 1Sam 15:22; Isa 1:11; Hos 6:6; Yer 6:20; Mt 9:13; Amo 5:22; Kut 21:6; Za 50:8; 51:16Dhabihu na sadaka hukuvitaka,

lakini umefungua masikio yangu;40:6 Au: bali mwili uliniandalia.

sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi

hukuzihitaji.

740:7 Ay 19:23; Yn 5:39; Yer 36:2; 45:1; Eze 2:9; Lk 24:44; Mdo 10:43; Ebr 10:7Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja:

imeandikwa kunihusu katika kitabu.

840:8 Mt 26:39; Yn 4:34; Ebr 10:5-7; Kum 6:6; Yer 15:16; Rum 7:22; Ay 22:22; 23:12Ee Mungu wangu,

natamani kuyafanya mapenzi yako;

sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”

940:9 Za 22:25, 31; 139:2; Yos 22:22Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa,

sikufunga mdomo wangu,

Ee Bwana, kama ujuavyo.

1040:10 Za 89:1; 22:22; Mdo 20:20; Flp 3:9; Rum 1:16, 17Sikuficha haki yako moyoni mwangu;

ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako.

Sikuficha upendo wako na kweli yako

mbele ya kusanyiko kubwa.

1140:11 Zek 1:12; Za 26:3; 61:7; 43:3; Mit 20:28Ee Bwana, usizuilie huruma zako,

upendo wako na kweli yako daima vinilinde.

1240:12 Za 25:17; 38:4; 65:3; 69:4; 73:26Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka,

dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona.

Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu,

nao moyo unazimia ndani yangu.

1340:13 Za 22:19; 38:22Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa;

Ee Bwana, njoo hima unisaidie.

1440:14 1Sam 20:1; Es 9:2; Za 35:26; 35:4Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,

waaibishwe na kufadhaishwa;

wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,

warudishwe nyuma kwa aibu.

1540:15 Za 35:21Wale waniambiao, “Aha! Aha!”

wafadhaishwe na iwe aibu yao.

1640:16 Kum 4:29; 1Nya 28:9; Za 9:10; 119:2; 9:2; 35:27Lakini wote wakutafutao

washangilie na kukufurahia,

wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,

Bwana atukuzwe!”

1740:17 Neh 5:19; Mk 10:21; Za 86:1; 109:22; 144:3; 20:2; 18:2; 119:60Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;

Bwana na anifikirie.

Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu;

Ee Mungu wangu, usikawie.