Zaburi 38 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 38:1-22

Zaburi 38

Maombi Ya Mtu Anayeteseka

Zaburi ya Daudi. Maombi.

138:1 Za 6:1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako,

wala kuniadhibu katika ghadhabu yako.

238:2 Ay 6:4Kwa kuwa mishale yako imenichoma,

na mkono wako umenishukia.

338:3 Mit 3:8; 4:22; Ay 33:19Hakuna afya mwilini mwangu

kwa sababu ya ghadhabu yako,

mifupa yangu haina uzima

kwa sababu ya dhambi zangu.

438:4 Za 40:12; 65:3; Hes 11:14; Ezr 9:6; Lk 11:46Maovu yangu yamenifunika

kama mzigo usiochukulika.

538:5 Za 147:3; Ay 19:17; Za 69:5; Mit 5:23; 12:23; 13:16; Mhu 10:3Majeraha yangu yameoza na yananuka,

kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.

638:6 Za 57:6; 145:14; 146:8; 35:14Nimeinamishwa chini na kushushwa sana,

mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.

738:7 Ay 14:22; 7:5Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo,

hakuna afya mwilini mwangu.

838:8 Za 6:3, 6; 22:1; 34:18; Mit 17:22; 5:11Nimedhoofika na kupondwa kabisa,

nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni.

938:9 Za 119:20; 143:7; Ay 3:24Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku

yako wazi mbele zako,

kutamani kwangu sana

hakufichiki mbele zako.

1038:10 Ay 37:1; Za 6:7; 31:10; 19:8; 88:9Moyo wangu unapigapiga,

nguvu zangu zimeniishia;

hata macho yangu yametiwa giza.

1138:11 Za 38:5; Lk 10:31Rafiki na wenzangu wananikwepa

kwa sababu ya majeraha yangu;

majirani zangu wanakaa mbali nami.

1238:12 Za 35:4, 20; 140:5; 31:4; 141:9; 41:5Wale wanaotafuta uhai wangu

wanatega mitego yao,

wale ambao wangetaka kunidhuru

huongea juu ya maangamizi yangu;

hufanya shauri la hila mchana kutwa.

1338:13 Za 115:6; 135:17; Isa 43:8; Mk 7:37Mimi ni kama mtu kiziwi, asiyeweza kusikia,

ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake,

14nimekuwa kama mtu asiyesikia,

ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu.

1538:15 Za 27:14; 17:6; Yer 14:8Ee Bwana, ninakungojea wewe,

Ee Bwana Mungu wangu, utajibu.

1638:16 Za 22:17; Kum 32:35Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie,

wala wasijitukuze juu yangu

mguu wangu unapoteleza.”

1738:17 Za 37:24; 38:7; Ay 6:10Kwa maana ninakaribia kuanguka,

na maumivu yangu yananiandama siku zote.

1838:18 Law 26:40; Ay 31:33; Za 32:5; Mit 28:13; 2Kor 7:9Naungama uovu wangu,

ninataabishwa na dhambi yangu.

1938:19 Za 18:17; 25:19; 35:19Wengi ni wale ambao ni adui zangu hodari,

wale wanaonichukia bila sababu ni wengi.

2038:20 Mwa 44:4; Yn 3:12; 1Pet 3:13; Za 54:5; 59:10; 119:23; 1Yn 3:12Wanaolipa maovu kwa wema wangu

hunisingizia ninapofuata lililo jema.

2138:21 Za 22:1, 11; 27:9; 71:18; 119:8; 10:1; 35:22; 71:12Ee Bwana, usiniache,

usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu.

2238:22 Za 22:19; 40:13; 1Nya 16:35; Kut 15:2; Isa 12:2Ee Bwana Mwokozi wangu,

uje upesi kunisaidia.