Zaburi 36 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 36:1-12

Zaburi 36

Uovu Wa Mwanadamu

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana.

136:1 Ay 21:16; 23:15; Yer 2:19; 36:16, 24; Rum 3:18; Mit 8:13; Mwa 20:11; Mhu 12:3Kuna neno moyoni mwangu

kuhusu hali ya dhambi ya mwovu.

Hakuna hofu ya Mungu

mbele ya macho yake.

236:2 Kum 29:19Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno

hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake.

336:3 Yer 4:22; 13:23; Za 10:7; 5:6, 9; 43:1; 144:8, 11; 94:8; Ay 5:13; Isa 44:20; Amo 3:10Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu,

ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema.

436:4 Mik 2:1; Rum 12:9; Isa 65:2; Za 52:3Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya,

hujitia katika njia ya dhambi

na hakatai lililo baya.

536:5 Za 89:1; 119:90; 108:4; 57:10; 89:2; 71:19; 103:11Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni,

uaminifu wako hadi kwenye anga.

636:6 Za 5:8; 68:15; Mwa 1:2; Za 104:14; 7:11; 145:9; Neh 9:6; Rum 11:33; Ay 7:20; 11:8Haki yako ni kama milima mikubwa,

hukumu zako ni kama kilindi kikuu.

Ee Bwana, wewe huwahifadhi

mwanadamu na mnyama.

736:7 Za 6:4; 17:8; 57:1; 91:4; Rut 2:12Upendo wako usiokoma

ni wa thamani mno!

Watu wakuu na wadogo

hujificha uvulini wa mbawa zako.

836:8 Za 65:4; 23:2; 63:5; Yer 31:12, 14; Ufu 22:1; Isa 25:6; Ay 20:17Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako,

nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako.

936:9 Isa 12:3; 2:5; 9:2; 60:1, 19; Yer 2:13; Zek 13:1; Yn 1:4; 4:10, 14; Ufu 21:6; Mdo 26:18; Efe 5:8; Kol 1:13; 1Pet 2:9; Mit 10:11; 16:22; Za 87:7; 4:6; 27:1; 76:4; 104:2Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima,

katika nuru yako twaona nuru.

1036:10 Yer 31:3; 9:24; 22:16; Za 7:10; 11:2; 94:15; 125:4Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe,

haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo.

1136:11 Za 71:4; 140:4Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu,

wala mkono wa mwovu usinifukuze.

1236:12 Za 18:38Angalia jinsi watenda mabaya walivyoanguka:

wametupwa chini, hawawezi kuinuka!