Zaburi 33 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 33:1-22

Zaburi 33

Ukuu Na Wema Wa Mungu

133:1 Za 64:10; 101:1; 147:1; 11:7Mwimbieni Bwana kwa furaha, enyi wenye haki;

kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.

233:2 Mwa 4:21; 1Kor 14:7; Ufu 5:8; Za 92:3; 144:9Msifuni Bwana kwa kinubi,

mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi.

333:3 Za 40:3; 35:27; 47:1; Isa 42:10; Ufu 5:9; Ay 3:7Mwimbieni wimbo mpya;

pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe.

433:4 Ufu 19:9; 22:6; Za 19:8; 18:25; 119:142; 25:10Maana neno la Bwana ni haki na kweli,

ni mwaminifu kwa yote atendayo.

533:5 Za 11:7; 6:4Bwana hupenda uadilifu na haki;

dunia imejaa upendo wake usiokoma.

633:6 Ebr 11:3; Kut 8:19; Mwa 1:3, 16; 2Nya 2:12; Yn 1:1-3; Ay 26:13Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa,

jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.

733:7 Mwa 1:10; Yos 3:16Ameyakusanya maji ya bahari

kama kwenye chungu;

vilindi vya bahari

ameviweka katika ghala.

833:8 Kum 6:13; 14:23; Za 2:11; 49:1; Isa 18:3; Mik 1:2Dunia yote na imwogope Bwana,

watu wote wa dunia wamche.

933:9 Za 148:5; Mwa 1:3Kwa maana Mungu alisema, na ikawa,

aliamuru na ikasimama imara.

1033:10 Isa 44:25; Za 2:1; Ay 5:12Bwana huzuia mipango ya mataifa,

hupinga makusudi ya mataifa.

1133:11 Hes 23:19; Yer 51:12, 29; Ay 23:13; Mit 19:21; Eze 38:10; Mdo 4:27, 28Lakini mipango ya Bwana inasimama imara milele,

makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote.

1233:12 Za 144:15; 65:4; 4:3; 84:4; Kum 7:6; Kut 8:22; 34:9Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,

watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake.

1333:13 Za 53:2; 102:19; 11:4; 14:2; Ebr 4:13; 2Nya 16:9; Ay 28:24Kutoka mbinguni Bwana hutazama chini

na kuwaona wanadamu wote;

1433:14 Law 15:31; 1Fal 8:39kutoka maskani mwake huwaangalia

wote wakaao duniani:

1533:15 Ay 10:8; 11:11; 10:4; Yer 32:19; Isa 64:8; Hes 7:2; Za 44:21; 119:73; Mit 24:12yeye ambaye huumba mioyo yao wote,

ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda.

1633:16 1Sam 14:6Hakuna mfalme aokokaye kwa ukubwa wa jeshi lake;

hakuna shujaa aokokaye kwa wingi wa nguvu zake.

1733:17 Za 20:7Farasi ni tumaini la bure kwa wokovu,

licha ya nguvu zake nyingi, hawezi kuokoa.

1833:18 Kut 3:16; Ay 36:7; Za 11:4; 6:4; 34:15; 1Pet 3:12Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao,

kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo,

1933:19 Za 56:13; Ay 5:20; Mdo 12:11ili awaokoe na mauti,

na kuwahifadhi wakati wa njaa.

2033:20 Za 27:14Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini,

yeye ni msaada wetu na ngao yetu.

2133:21 1Sam 2:1; Yoe 2:23; Za 30:4; 99:3Mioyo yetu humshangilia,

kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu.

2233:22 Za 6:4Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana,

tunapoliweka tumaini letu kwako.