Zaburi 30 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 30:1-12

Zaburi 30

Maombi Ya Shukrani

Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi.

130:1 Kut 15:2; Isa 14:15; Ay 11:8; Mit 9:18; Za 63:9; 107:26; 22:17Nitakutukuza wewe, Ee Bwana,

kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,

na hukuacha adui zangu

washangilie juu yangu.

230:2 Za 5:2; 88:13; 6:2-4; Hes 12:13Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie

na wewe umeniponya.

330:3 Za 40:1, 2; 16:10; 56:13; 28:1; 55:23; 69:15; 86:13; 143:7; Mit 1:12; Isa 38:17; Yon 2:6Ee Bwana, umenitoa Kuzimu,

umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.

430:4 Za 33:1; 47:7; 68:4; 16:3; 33:21; 103:1; 145:21; Kut 3:15Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake;

lisifuni jina lake takatifu.

530:5 Za 103:9; 126:6; 6:6; 2Sam 15:30; 2Kor 4:17; Ezr 3:1; Ay 14:13; Yer 31:6Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,

bali upendo wake hudumu siku zote.

Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,

lakini asubuhi kukawa na furaha.

630:6 Ay 29:18Nilipofanikiwa nilisema,

“Sitatikiswa kamwe.”

730:7 Kum 31:17; Za 104:29Ee Bwana, uliponijalia,

uliuimarisha mlima wangu,

lakini ulipouficha uso wako

nilifadhaika.

8Kwako wewe, Ee Bwana, niliita,

kwa Bwana niliomba rehema:

930:9 Ay 33:18; Isa 38:18; Za 6:5; 88:11; 115:17“Kuna faida gani katika kuangamia kwangu?

Katika kushuka kwangu shimoni?

Je, mavumbi yatakusifu?

Je, yatatangaza uaminifu wako?

1030:10 Za 17:1; 4:1; 20:2Ee Bwana, unisikie na kunihurumia,

Ee Bwana, uwe msaada wangu.”

1130:11 2Sam 3:31; 6:14; Es 4:1; Kut 15:20; Za 35:13; 16:9; Kum 16:15Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza,

ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,

1230:12 Za 35:18; 75:1; 118:21; 44:8; 52:9; Ufu 11:17ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya.

Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.