Zaburi 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 3:1-8

Zaburi 3

Sala Ya Asubuhi Ya Kuomba Msaada

Zaburi ya Daudi. Alipomkimbia mwanawe Absalomu.

13:1 1Sam 15:12Ee Bwana, tazama adui zangu walivyo wengi!

Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!

23:2 Za 22:8; 22:7, 8; 71:11Wengi wanasema juu yangu,

“Mungu hatamwokoa.”

33:3 Mwa 15:1; Za 27:6; 2Fal 25:27Lakini wewe, Ee Bwana, ni ngao pande zote;

umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.

43:4 Ay 30:20; Za 2:6; 27:6Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu,

naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.

53:5 Law 26:6; Mdo 12:6; Za 4:8; 17:15; 139:18; Mit 3:24Ninajilaza na kupata usingizi;

naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza.

63:6 Za 23:4; 27:3; 118:11; Ay 11:15Sitaogopa makumi elfu ya adui,

wanaojipanga dhidi yangu kila upande.

73:7 2Nya 6:41; Mt 6:13; Za 6:4; 7:1; 59:1; 57:4; 109:21; 119:153; Isa 25:9; 33:22; 35:4; 36:15; 37:20; Yer 42:11; Mao 3:16; Ay 16:10; 29:17; Mit 30:14Ee Bwana, amka!

Niokoe, Ee Mungu wangu!

Wapige adui zangu wote kwenye taya,

vunja meno ya waovu.

83:8 Za 27:1; 37:39; 62:1; Hes 6:23; Isa 43:3, 11; 44:6, 8; 45:21; Hos 13:4; Yon 2:9; Mit 21:31; Za 29:11; 129:8Kwa maana wokovu watoka kwa Bwana.

Baraka yako na iwe juu ya watu wako.