Zaburi 23 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 23:1-6

Zaburi 23

Bwana Mchungaji Wetu

Zaburi ya Daudi.

123:1 Mwa 48:15; Yn 10:11; Flp 4:19; Za 28:9; 34:9, 10; 84:11; 107:9; 1Pet 2:25Bwana ndiye mchungaji wangu,

sitapungukiwa na kitu.

223:2 Eze 34:14; Ufu 7:17; Za 36:8; 46:4Hunilaza katika malisho

ya majani mabichi,

kando ya maji matulivu huniongoza,

323:3 Isa 42:16; Za 5:8; 106:8; 19:7; 79:9; 25:9, 11; 73:24; 31:3; 109:21; 143:11hunihuisha nafsi yangu.

Huniongoza katika njia za haki

kwa ajili ya jina lake.

423:4 Ay 3:5; Za 107:14; Isa 43:2; Za 3:6; 27:1; 16:8; 46:11; Isa 8:10; Zek 8:23; Mt 1:23; Mdo 18:9, 10Hata kama nikipita katikati

ya bonde la uvuli wa mauti,

sitaogopa mabaya,

kwa maana wewe upo pamoja nami;

fimbo yako na mkongojo wako

vyanifariji.

523:5 Ay 36:16; Za 16:5; 45:7; 92:10; Lk 7:46Waandaa meza mbele yangu

machoni pa adui zangu.

Umenipaka mafuta kichwani pangu,

kikombe changu kinafurika.

623:6 Neh 9:25; 2Kor 5:1Hakika wema na upendo vitanifuata

siku zote za maisha yangu,

nami nitakaa nyumbani mwa Bwana

milele.