Zaburi 21
Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Ushindi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
121:1 1Sam 2:10; 2Sam 22:51Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako.
Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake
kwa ushindi unaompa!
221:2 Za 20:4; Yn 11:42Umempa haja ya moyo wake
na hukumzuilia maombi ya midomo yake.
321:3 2Sam 12:30; Ufu 14:14; Zek 6:11Ulimkaribisha kwa baraka tele
na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
421:4 Za 10:16; 45:17; 48:14; 133:3; 2Sam 7:19Alikuomba maisha, nawe ukampa,
wingi wa siku milele na milele.
521:5 Za 18:50; 44:4; 8:5; 45:3; 93:1; 96:6; 104:1Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa,
umeweka juu yake fahari na utukufu.
621:6 Za 43:4; 126:3; 1Nya 17:27Hakika umempa baraka za milele,
umemfanya awe na furaha
kwa shangwe ya uwepo wako.
721:7 2Fal 18:5; Za 6:4; 15:5; 55:22; 91:7; Mwa 14:18Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana;
kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.
821:8 Isa 10:10Mkono wako utawashika adui zako wote,
mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.
921:9 Kum 32:22; Yer 15:14Wakati utakapojitokeza
utawafanya kama tanuru ya moto.
Katika ghadhabu yake Bwana atawameza,
moto wake utawateketeza.
1021:10 Kum 28:18Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani,
uzao wao kutoka wanadamu.
1121:11 Za 2:1; 10:2; 26:10; 37:7; Ay 10:3Ingawa watapanga mabaya dhidi yako
na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,
1221:12 Kut 23:27kwa kuwa utawafanya wakimbie
utakapowalenga usoni pao
kwa mshale kutoka kwenye upinde wako.
1321:13 Za 18:46; Ufu 15:3, 4Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako,
tutaimba na kusifu nguvu zako.