Zaburi 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 2:1-12

Zaburi 2

Mfalme Aliyechaguliwa Na Mungu

12:1 Za 21:11; 83:5; Mit 24:2Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya,

na kabila za watu kula njama bure?

22:2 Za 45:7; 48:4; 1Sam 9:16; Yn 1:41; Mdo 4:25-262:2 Mao 3:55; Za 22:2; 55:17; 142:5; 42:7Wafalme wa dunia wanajipanga

na watawala wanajikusanya pamoja

dhidi ya Bwana

na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.

32:3 Ay 36:8; Lk 19:14; 2Sam 3:34Wanasema, “Tuvunje minyororo yao

na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”

42:4 Za 11:4; Isa 37:16; 40:22; 66:1; Za 37:13; Mit 1:26Yeye atawalaye mbinguni hucheka,

Bwana huwadharau.

52:5 Za 6:1; 27:9; 38:1; 21:9; 79:6; 90:7; 110:5Kisha huwakemea katika hasira yake

na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,

62:6 Za 10:16; 24:10; 9:11; 48:2, 11; 78:6; 110:2; 133:3; 2Fal 19:31; Kut 15:17“Nimemtawaza Mfalme wangu

juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”

Ushindi Wa Mfalme

72:7 Mt 3:17; 8:29; 2Sam 7:14; Ebr 1:5; 5:5; Mdo 13:33Nitatangaza amri ya Bwana:

Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu,

leo mimi nimekuzaa.

82:8 Ay 22:26; Za 22:27; 67:7; Dan 7:13, 14; Mt 21:38Niombe, nami nitayafanya mataifa

kuwa urithi wako,

miisho ya dunia kuwa milki yako.

92:9 Mwa 49:10; Ufu 2:27; 12:5; 19:15; Mt 21:44; Kut 15:6; Isa 30:14; Yer 19:10Utawatawala kwa fimbo ya chuma

na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”

102:10 Za 141:6; Amu 2:3; Mit 8:15; 27:11Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima;

mwonyeke, enyi watawala wa dunia.

112:11 1Nya 16:30; Za 9:2; 35:9; Isa 61:10Mtumikieni Bwana kwa hofu

na mshangilie kwa kutetemeka.

122:12 Kum 9:8; Za 5:11; 34:8; 64:10; Yer 17:7; Ufu 6:16; Yn 5:22, 23Mbusu Mwana, asije akakasirika

nawe ukaangamizwa katika njia yako,

kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula.

Heri wote wanaomkimbilia.