Zaburi 18 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 18:1-50

Zaburi 18

Wimbo Wa Daudi Wa Ushindi

(2 Samweli 22:1-51)

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana aliyomwimbia Bwana wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. Alisema hivi:

118:1 Kut 15:2; Yer 16:19; Kum 32:4; 33:29; Za 91:2; 22:19; 59:9; 81:1; 1Sam 2:2; Isa 2:10; 12:2; 49:5Nakupenda wewe, Ee Bwana,

nguvu yangu.

218:2 Kut 33:22; Isa 2:1; 17:10; Yer 16:19; Za 40:17; 114:2; 2:12; 9:9; 94:20; 28:7, 8; 31:2, 3; 84:9; 119:114; Ebr 2:13; Mwa 15:1; Lk 1:69Bwana ni mwamba wangu,

ngome yangu na mwokozi wangu,

Mungu wangu ni mwamba,

ambaye kwake ninakimbilia.

Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu,

ngome yangu.

318:3 1Nya 16:25; Za 9:13; 76:4Ninamwita Bwana anayestahili kusifiwa,

nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.

418:4 Za 116:4; 93:4; 124:6; Eze 43:2; Isa 5:30; 17:12; Yer 6:23; 51:42, 55Kamba za mauti zilinizunguka,

mafuriko ya maangamizi yalinilemea.

518:5 Mit 14:13Kamba za kuzimu zilinizunguka,

mitego ya mauti ilinikabili.

618:6 Kum 4:30; Za 30:2; 99:6; 102; 120:1; 66:19; 116:1; Ay 16:18Katika shida yangu nalimwita Bwana,

nilimlilia Mungu wangu anisaidie.

Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu,

kilio changu kikafika mbele zake,

masikioni mwake.

718:7 Za 97:4; Isa 5:25; 64:3; Amu 5:4, 5; Ay 9:5; Yer 10:10; Mdo 4:31Dunia ilitetemeka na kutikisika,

misingi ya milima ikatikisika,

vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.

818:8 Ay 41:20, 21; Kut 15:17; 19:18; Mit 25:22; Za 50:3; 97:3; Dan 7:10; Rum 12:20Moshi ukapanda kutoka puani mwake,

moto uteketezao ukatoka kinywani mwake,

makaa ya moto yawakayo

yakatoka ndani mwake.

918:9 Mwa 11:5; Isa 64:1; Za 57:3; 104:3; Kut 20:21; Kum 33:26Akazipasua mbingu akashuka chini,

mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.

1018:10 Mwa 3:24; Eze 10:18; Kum 33:26; Za 104:3; 99:1Alipanda juu ya kerubi akaruka,

akapaa juu kwa mbawa za upepo.

1118:11 Za 97:2; Kut 19:9; Ay 22:14; Isa 4:5; Kum 4:11; Yer 43:10Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika,

hema lake kumzunguka,

mawingu meusi ya mvua ya angani.

1218:12 Za 104:2; Yos 10:10; Ay 36:30Kutokana na mwanga wa uwepo wake

mawingu yalisogea,

ikanyesha mvua ya mawe

na umeme wa radi.

1318:13 Kut 9:23; Za 29:3; 2Sam 2:10Bwana alinguruma kutoka mbinguni,

sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.

1418:14 Kum 32:23; Ay 6:4; 36:30; Ufu 4:5; Za 21:12; Amu 4:15; Hes 24:8Aliipiga mishale yake na kutawanya adui,

naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.

1518:15 Za 11:3; 76:6; 104:7; 106:9; Isa 50:2; Kut 15:8Mabonde ya bahari yalifunuliwa,

na misingi ya dunia ikawa wazi

kwa kukaripia kwako, Ee Bwana,

kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako.

1618:16 Kut 15:5; Mit 18:4; 20:5; Za 69:2; 144:7Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika;

alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.

1718:17 Za 38:19; 59:1; 143:9; Amu 18:26Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi,

kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.

1818:18 Mit 1:27; 16:4; Yer 17:17; 40:2; Oba 1:13; Za 20:2; Isa 3:1Walinikabili siku ya msiba wangu,

lakini Bwana alikuwa msaada wangu.

1918:19 Za 31:8; 118:5; Hes 14:8Alinileta nje mahali penye nafasi tele,

akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.

2018:20 1Sam 22:21; 26:23; Ay 22:30; Za 24:4; Rum 2:12; 2Nya 15:7; 1Kor 3:8; Mit 6:4Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu;

sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.

2118:21 2Nya 34:33; Za 37:34; 119:2; 102; Mit 8:32; 23:26Kwa maana nimezishika njia za Bwana;

sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.

2218:22 Za 119:30Sheria zake zote zi mbele yangu,

wala sijayaacha maagizo yake.

2318:23 Mwa 6:9Nimekuwa sina hatia mbele zake,

nami nimejilinda nisitende dhambi.

2418:24 1Sam 26:23; Rut 2:12; Mt 10:41-42Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu;

sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake.

2518:25 Za 31:23; 37:23; 50:5; 25:10; 40:11; 89:24; 146:6; Mit 2:8; Mt 18:32-35Kwa yeye aliye mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu,

kwa asiye na hatia, unajionyesha kutokuwa na hatia.

2618:26 Mit 15:26; Mt 5:8; Flp 1:10; 1Tim 5:22; Tit 1:15; 1Yn 3:3; Mit 3:34; Mt 10:16; Lk 16:8; Law 26:23Kwa aliye mtakatifu, unajionyesha kuwa mtakatifu,

lakini kwa aliyepotoka, unajionyesha kuwa mkaidi.

2718:27 2Nya 33:23; Mt 23:12; Ay 41:34; Za 10:5; Mit 3:33-35; 6:17Wewe huwaokoa wanyenyekevu,

lakini huwashusha wenye kiburi.

2818:28 1Fal 11:36; Za 132:17; Ay 29:3; Za 97:11; 112:4; Yn 1:5; Mdo 26:18; 2Kor 4:6; 2Pet 1:19; Ay 18:6Wewe, Ee Bwana, unaifanya taa yangu iendelee kuwaka;

Mungu wangu hulifanya giza langu kuwa mwanga.

2918:29 Isa 45:5; Ebr 11:34Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi,

nikiwa pamoja na Mungu wangu

nitaweza kuruka ukuta.

3018:30 Kum 32:4; Za 12:6; 3:3; 2:12; Mit 30:5; Ufu 15:3; Rum 12:3Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu,

neno la Bwana halina dosari.

Yeye ni ngao kwa wote

wanaokimbilia kwake.

3118:31 Kum 4:5; 32:39; Za 35:10; 86:8; 89:6; Isa 46:9; 44:6, 8; 45:5, 6, 14, 18, 21; Mwa 49:24Kwa maana ni nani aliye Mungu

zaidi ya Bwana?

Ni nani aliye Mwamba

isipokuwa Mungu wetu?

3218:32 1Pet 5:10; Yak 3:2; Za 15:2; 19:13; Ebr 10:14Mungu ndiye anivikaye nguvu

na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.

3318:33 Za 42:1; Mit 5:19; Isa 35:6; Hab 3:19; Kum 32:13Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu,

huniwezesha kusimama mahali palipo juu.

3418:34 Za 144:1Huifundisha mikono yangu kupigana vita;

mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.

3518:35 Za 3:5; 37:5, 17; 41:3; 51:2; 54:4; 55:22; 119:116; Isa 41:4, 10, 13; 43:2; 46:4Hunipa ngao yako ya ushindi,

nao mkono wako wa kuume hunitegemeza,

unajishusha chini ili kuniinua.

3618:36 Ay 18:7; Za 31:8; 66:9Huyapanua mapito yangu,

ili miguu yangu isiteleze.

3718:37 Law 26:7Niliwafuatia adui zangu na nikawapata,

sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.

3818:38 Za 68:21; 110:6; 36:12; 47:3; 140:10; Isa 26:14Niliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena;

walianguka chini ya miguu yangu.

3918:39 Za 18:32, 47; Isa 45:5, 24; Za 47:3; 144:2Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita;

uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.

4018:40 Yos 7:12; Za 18:37Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia,

nami nikawaangamiza adui zangu.

4118:41 2Fal 14:26; Za 50:22; 1Sam 8:18; 14:37; Yer 11:11; Mit 1:28Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa;

walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu.

4218:42 Kum 9:21; Isa 2:22Niliwaponda kama mavumbi yanayopeperushwa na upepo;

niliwamwaga nje kama tope barabarani.

4318:43 2Sam 8:1-14; Isa 55:5Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu;

umenifanya kuwa kiongozi wa mataifa,

watu ambao sikuwajua wananitumikia.

4418:44 Za 144:7, 11; 54:3; Isa 25:5Mara wanisikiapo hunitii,

wageni hunyenyekea mbele yangu.

4518:45 2Kor 4:1; Ebr 12:3; 1Sam 17:32; Isa 66:2; Hos 3:5; 11:10; Za 9:9; Mik 7:17Wote wanalegea,

wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.

4618:46 Yos 3:10; 2Kor 13:4; 1Sam 14:39; Kut 33:22; Za 21:13; 35:27; 40:16; 108:5; 1Nya 16:35; Lk 1:47; Yer 10:10Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu!

Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu!

4718:47 Mwa 4:24; Za 18:29; Amu 4:23Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi,

awatiishaye mataifa chini yangu,

4818:48 Dan 3:17; Za 7:10; 37:40; 140:2; 18:49aniokoaye na adui zangu.

Uliniinua juu ya adui zangu;

uliniokoa toka kwa watu wajeuri.

4918:49 Za 101:1; 7:17; 9:2; 108:1; 146:2; Rum 15:9Kwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, Ee Bwana;

nitaliimbia sifa jina lako.

5018:50 2Sam 23:1; Za 144:10; 89:4Humpa mfalme wake ushindi mkuu,

huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake,

kwa Daudi na wazao wake milele.