Zaburi 17 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 17:1-15

Zaburi 17

Sala Ya Mtu Asiye Na Hatia

Sala ya Daudi.

117:1 Za 30:10; 64:1; 80:1; 140:6; 5:1, 2; 39:12; 142:6; 143:1; Isa 29:13Sikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki,

sikiliza kilio changu.

Tega sikio kwa ombi langu,

halitoki kwenye midomo ya udanganyifu.

217:2 Za 24:5; 26:1; 99:4; Isa 46:13; 50:8-9; 54:17Hukumu yangu na itoke kwako,

macho yako na yaone yale yaliyo haki.

317:3 Za 139:1; Yak 3:2; Ay 7:18; 23:10; Yer 12:3; 50:20Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku,

ingawa umenijaribu, hutaona chochote.

Nimeamua kwamba kinywa changu

hakitatenda dhambi.

417:4 Rum 12:2Kuhusu matendo ya wanadamu:

kwa neno la midomo yako,

nimejiepusha

na njia za wenye jeuri.

517:5 Ay 23:11; Za 44:18; 73:2; 121:3; Kum 32:35Hatua zangu zimeshikamana na njia zako;

nyayo zangu hazikuteleza.

617:6 Za 84:7; 116:2; 4:1Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu,

nitegee sikio lako na usikie ombi langu.

717:7 Za 31:21; 69:13; 106:45; 107:43; 117:2; 10:12; 2:12Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu,

wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume

wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.

817:8 Hes 6:24; Isa 34:15; Kum 32:10; Mit 7:2; Za 27:5; 31:20; 32:7; 36:7; 63:7; Rum 2:12Nilinde kama mboni ya jicho lako,

unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako

917:9 Za 109:3kutokana na waovu wanaonishambulia,

kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.

1017:10 Za 73:7; 119:70; Isa 6:10; 2:3Huifunga mioyo yao iliyo migumu,

vinywa vyao hunena kwa majivuno.

1117:11 Za 88:17; 1Sam 23:26Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira,

wakiwa macho, waniangushe chini.

1217:12 Za 7:2; Yer 5:6; 12:8; Mao 3:10; Mwa 49:9Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye,

kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni.

1317:13 Za 35:8; 55:23; 73:18; Hes 10:3Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe,

niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako.

1417:14 Za 49:17; Lk 16:8, 25; Isa 2:7; 57:17Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii,

kutokana na watu wa ulimwengu huu

ambao fungu lao liko katika maisha haya.

Na wapate adhabu ya kuwatosha.

Watoto wao na wapate zaidi ya hayo,

hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.

1517:15 Za 3:5; Hes 12:2; Mt 5:8; 1Yn 3:2Na mimi katika haki nitauona uso wako,

niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.