Zaburi 15 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 15:1-5

Zaburi 15

Kitu Mungu Anachotaka

Zaburi ya Daudi.

115:1 Za 27:4; 23:6; 2:5; 61:4; 20:2; 78:69; 150:1; Kut 29:46; 25:8; 15:17; 1Nya 22:19Bwana, ni nani awezaye kukaa

katika Hekalu lako?

Nani awezaye kuishi

katika mlima wako mtakatifu?

215:2 1The 3:13; Tit 1:6; Mit 16:13; Rum 9:1; Isa 38:15, 16; 45:19; Yer 7:28; 9:5; Mwa 6:9; Efe 1:4; 4:25; Za 18:32; 84:11; Zek 8:3, 16Ni yule aendaye pasipo mawaa,

atendaye yaliyo haki,

asemaye kweli toka moyoni mwake,

315:3 Law 19:16na hana masingizio ulimini mwake,

asiyemtenda jirani yake vibaya,

na asiyemsingizia mwenzake,

415:4 Ay 19:9; Yos 9:18; Mdo 28:10; Kum 23:21; Mt 5:33ambaye humdharau mtu mbaya,

lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana,

yule atunzaye kiapo chake

hata kama anaumia.

515:5 Kut 22:25; 18:21; Mdo 24:26; 2Pet 1:10; Za 21:7; 112:6; Ay 29:18; Ebr 12:28Yeye akopeshaye fedha yake bila riba,

na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.

Mtu afanyaye haya

kamwe hatatikisika.