Zaburi 148 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 148:1-14

Zaburi 148

Mwito Kwa Ulimwengu Kumsifu Mungu

1148:1 Za 33:2; 103; 1; 19:1; 69:34; 150:1Msifuni Bwana.

Msifuni Bwana kutoka mbinguni,

msifuni juu vileleni.

2148:2 Za 103:20; 1Fal 22:19; Dan 7:10; Ebr 1:7Msifuni, enyi malaika wake wote,

msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.

3148:3 Za 19:1Msifuni yeye, enyi jua na mwezi,

msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo.

4148:4 Kum 10:14; Mwa 1:7; 1Fal 8:27Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana,

na ninyi maji juu ya anga.

5148:5 Za 145:21; 147:15; Ebr 11:3Vilisifu jina la Bwana

kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.

6148:6 Yer 31:35-36; 33:25; 33:25Aliviweka mahali pake milele na milele,

alitoa amri ambayo haibadiliki milele.

7148:7 Za 33:2; 74:13, 14; Mwa 1:21; Isa 43:20; Kum 33:13Mtukuzeni Bwana kutoka duniani,

ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari,

8148:8 Yos 10:11; Ay 37:11, 12; Za 147:15-18; 103:20; Kut 9:18umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu,

pepo za dhoruba zinazofanya amri zake,

9148:9 Isa 44:23; 49:13; 55:12ninyi milima na vilima vyote,

miti ya matunda na mierezi yote,

10148:10 Isa 43:20; Hos 2:18wanyama wa mwituni na mifugo yote,

viumbe vidogo na ndege warukao,

11148:11 Za 102:15; Mdo 17:28wafalme wa dunia na mataifa yote,

ninyi wakuu na watawala wote wa dunia,

12wanaume vijana na wanawali,

wazee na watoto.

13148:13 Za 113:2; 138:4; 145:5; 8:1; Isa 6:3; Flp 2:9Wote na walisifu jina la Bwana,

kwa maana jina lake pekee limetukuka,

utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.

14148:14 Kut 15:2; 1Pet 2:9; Za 22:3; 145:10; Kum 26:19; Efe 2:17; 1Sam 1:2Amewainulia watu wake pembe,148:14 Pembe hapa inawakilisha mwenye nguvu, yaani mfalme.

sifa ya watakatifu wake wote,

ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake.

Msifuni Bwana.