Zaburi 147 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 147:1-20

Zaburi 147

Kumsifu Mungu Mwenye Nguvu Zote

1147:1 Za 135:3; 33:1Msifuni Bwana.

Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa,

jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!

2147:2 Za 51:18; 106:47; Kum 30:3; Isa 27:13; Yer 32:37; Eze 36:24Bwana hujenga Yerusalemu,

huwakusanya Israeli walio uhamishoni.

3147:3 Za 34:18; Isa 1:6; 61:1; Eze 34:16; Ebr 12:13; Ay 5:18; Lk 4:18Anawaponya waliovunjika mioyo

na kuvifunga vidonda vyao.

4147:4 Mwa 15:5; Isa 40:26Huzihesabu nyota

na huipa kila moja jina lake.

5147:5 Kut 14:31; Nah 1:3; 1Nya 16:25; Za 48:1; 145:3; Isa 40:28Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi,

ufahamu wake hauna kikomo.

6147:6 2Nya 33:23; Za 146:8, 9; 37:9, 10; 145:20Bwana huwahifadhi wanyenyekevu

lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.

7147:7 Za 30:4; 33:3; 42:4; 27:6; 98:5; Efe 2:20Mwimbieni Bwana kwa shukrani,

mpigieni Mungu wetu kinubi.

8147:8 Kum 32:2; 11:14; 2Sam 1:21; Ay 26:8; 38:26; 5:10; 28:26; Za 104:14Yeye huzifunika anga kwa mawingu,

huinyeshea ardhi mvua,

na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima.

9147:9 Ay 38:41; Mt 6:26; Mwa 8:7; 1:30; Lk 12:24; Za 104:27, 28Huwapa chakula mifugo

na pia makinda ya kunguru yanapolia.

10147:10 1Sam 16:7; Hos 1:7; Ay 39:11; Za 33:16-17Furaha yake haipo katika nguvu za farasi,

wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu.

11147:11 Za 35:27; 33:18; 103:11; 119:43; 6:4Bwana hupendezwa na wale wamchao,

wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma.

12147:12 Za 48:1Mtukuze Bwana, ee Yerusalemu,

msifu Mungu wako, ee Sayuni,

13147:13 Kum 33:25; Law 25:21; Za 128:5; 134:3kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako

na huwabariki watu wako walio ndani yako.

14147:14 Law 26:6; 2Sam 7:10; Isa 48:18; Za 132:15; Kum 32:14Huwapa amani mipakani mwenu

na kukushibisha kwa ngano safi kabisa.

15147:15 Ay 37:12; Za 33:9; 148:5; Isa 55:11Hutuma amri yake duniani,

neno lake hukimbia kasi.

16147:16 Za 148:8; Ay 37:12; 38:29Anatandaza theluji kama sufu

na kutawanya umande kama majivu.

17147:17 Kut 9:22, 23; Ay 38:22; Za 78:47Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe.

Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake?

18147:18 Za 33:9; 107:20; 50:3Hutuma neno lake na kuviyeyusha,

huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka.

19147:19 Kut 20:1; Mal 4:4; Za 78:5; Yos 1:8; Kum 33:4; 2Fal 22:8; Rum 3:2; 9:4Amemfunulia Yakobo neno lake,

sheria zake na maagizo yake kwa Israeli.

20147:20 Rum 3:1-2; Kum 4:7-8, 32-34; Za 79:6; 103:1; 33:2; Mdo 14:16Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote,

hawazijui sheria zake.

Msifuni Bwana.