Zaburi 145 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 145:1-21

Zaburi 145145:1 Zaburi hii imetungwa kila mstari (ikiwa ni pamoja na 13b) ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.

Wimbo Wa Kusifu Ukuu Na Wema Wa Mungu

Wimbo wa Sifa. Wa Daudi.

1145:1 Za 30:1; 34:1; 2:6; 5:2; 54:6Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme,

nitalisifu jina lako milele na milele.

2145:2 Za 71:6; 34:1; Isa 25:1; 26:8Kila siku nitakusifu

na kulitukuza jina lako milele na milele.

3145:3 2Sam 22:4; Ay 5:9; Za 95:3; 96:4Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana,

ukuu wake haupimiki.

4145:4 Za 22:30; 71:16; Kum 11:19Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine,

watasimulia matendo yako makuu.

5145:5 Za 96:6; 148:13; 75:1Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako,

nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.

6145:6 Kum 32:3; Za 75:1; 78:4; 66:3; 106:2Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha,

nami nitatangaza matendo yako makuu.

7145:7 Kut 18:9; Za 5:11; 27:13; 138:5; 101:1Wataadhimisha wema wako mwingi,

na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.

8145:8 Za 57:10; 86:15; 103:8; Kut 34:6; Hes 14:18; Yn 1:17; Mao 3:22Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma,

si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo.

9145:9 1Nya 16:34; Mt 19:17; Nah 1:7; Mk 10:18; Mdo 14:17; Za 103:13, 14; 136:1; 100:5Bwana ni mwema kwa wote,

ana huruma kwa vyote alivyovifanya.

10145:10 Za 8:6; 103:22; 139:14; 148:14; 19:1; 149:9; 30:4; 115:17-18Ee Bwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu,

watakatifu wako watakutukuza.

11Watasimulia utukufu wa ufalme wako

na kusema juu ya ukuu wako,

12145:12 Za 103:19; 105:1; 75:1; Isa 2:10, 19, 21ili watu wote wajue matendo yako makuu

na utukufu wa fahari ya ufalme wako.

13145:13 Kut 15:18; 1Tim 1:17; 2Pet 1:11; Ufu 11:15; Kum 7:9; 1Kor 1:9; Yos 23:14Ufalme wako ni ufalme wa milele,

mamlaka yako hudumu vizazi vyote.

Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote

na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.

14145:14 Za 37:17; 146:8; 38:6; 1Sam 2:8Bwana huwategemeza wote waangukao,

na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.

15145:15 Mwa 1:30; Ay 28:5; Mt 6:26; Za 37:25Macho yao wote yanakutazama wewe,

nawe huwapa chakula chao wakati wake.

16145:16 Za 90:14; 104; 28Waufumbua mkono wako,

watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.

17145:17 Kut 9:27; Ezr 9:15Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote,

na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.

18145:18 Flp 4:5; Za 46:1; 18:6; 80:18; 91:1; Isa 61:10; Ufu 3:20; Yak 4:8; 1Yn 2:24; Yud 23; Yn 4:23; 14:23; Hes 23:21Bwana yu karibu na wote wamwitao,

karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.

19145:19 1Yn 5:14; Za 20:4; 31:22; 40:1; 7:10; 34:18; 1Sam 10:19; Ay 22:28Huwatimizia wamchao matakwa yao,

husikia kilio chao na kuwaokoa.

20145:20 Za 94:23; 31:23; 91:14; 97:10; 1:6; 1Pet 1:5Bwana huwalinda wote wampendao,

bali waovu wote atawaangamiza.

21145:21 Za 71:8; 65:2; 150:6; 30:4; 99:3; Kut 3:15Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana.

Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu

milele na milele.