Zaburi 144 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 144:1-15

Zaburi 144

Mfalme Amshukuru Mungu Kwa Ushindi

Zaburi ya Daudi.

1144:1 Mwa 49:24; 2Sam 22:35Sifa ni kwa Bwana Mwamba wangu,

aifundishaye mikono yangu vita,

na vidole vyangu kupigana.

2144:2 Za 59:9; 91:2; 18:39; 27:1; 37:39; 43:2; 18:2; Amu 4:23; Mwa 15:1Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu,

ngome yangu na mwokozi wangu,

ngao yangu ninayemkimbilia,

ambaye huwatiisha mataifa chini yangu.

3144:3 Ebr 2:6Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali,

Binadamu ni nini hata umfikirie?

4144:4 Ay 7:7; 27:3; 14:2; Isa 2:22; 1Nya 29:15; Yak 4:14Mwanadamu ni kama pumzi,

siku zake ni kama kivuli kinachopita.

5144:5 Za 18:9; 57:3; 104:32; Isa 64:1; Mwa 11:5Ee Bwana, pasua mbingu zako, ushuke,

gusa milima ili itoe moshi.

6144:6 Hab 3:11; Zek 9:14; Za 59:11; 68:1; 7:12, 13; 18:14Peleka umeme uwatawanye adui,

lenga mishale yako uwashinde.

7144:7 2Sam 22:17; Za 3:7; 57:3; 69:2; 18:44Nyoosha mkono wako kutoka juu,

nikomboe na kuniokoa

kutoka maji makuu,

kutoka mikononi mwa wageni

8144:8 Za 12:2; 41:6; 26:3; Mwa 14:22; Kum 32:40ambao vinywa vyao vimejaa uongo,

na mikono yao ya kuume ni midanganyifu.

9144:9 Za 28:7; 96:1; 33:2-3; 71:22; 69:1Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,

kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia,

10144:10 2Sam 8:14; Za 18:50; Ay 5:20kwa Yule awapaye wafalme ushindi,

ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake kutokana na upanga hatari.

11144:11 Za 3:7; 25:20; 18:44; 41:6-7; 12:2; 36:3; 106:26; Isa 44:20Nikomboe na uniokoe

kutoka mikononi mwa wageni

ambao vinywa vyao vimejaa uongo,

na mikono yao ya kuume ni midanganyifu.

12144:12 Za 92:12-14; 128:3; 4:4; 7:4Kisha wana wetu wakati wa ujana wao

watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri,

binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa

kurembesha jumba la kifalme.

13144:13 Mit 3:10Ghala zetu zitajazwa

aina zote za mahitaji.

Kondoo zetu watazaa kwa maelfu,

kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu;

14144:14 Mit 14:4; 2Fal 25:11; Isa 24:11; Yer 14:2-3; Law 26:17maksai wetu watakokota

mizigo mizito.

Hakutakuwa na kubomoka kuta,

hakuna kuchukuliwa mateka,

wala kilio cha taabu

katika barabara zetu.

15144:15 Kum 28:3; 33:29Heri watu ambao hili ni kweli;

heri wale ambao Bwana ni Mungu wao.