Zaburi 143 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 143:1-12

Zaburi 143

Maombi Ya Kuokolewa Dhidi Ya Adui

Zaburi ya Daudi.

1143:1 Za 141:1; 28:2; 130:2; 89:1-2Ee Bwana, sikia sala yangu,

sikiliza kilio changu unihurumie;

katika uaminifu na haki yako

njoo unisaidie.

2143:2 Za 14:3; Rum 3:10; Ay 14:3; 4:17; Mhu 7:20; Gal 2:16Usimhukumu mtumishi wako,

kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako.

3143:3 Za 107:10; 7:1, 2; Law 3:6Adui hunifuatilia,

hunipondaponda chini;

hunifanya niishi gizani

kama wale waliokufa zamani.

4143:4 Za 30:7Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu,

moyo wangu ndani yangu unakata tamaa.

5143:5 Za 77:6; 77:5, 11; Mwa 24:63Nakumbuka siku za zamani;

natafakari juu ya kazi zako zote,

naangalia juu ya kazi

ambazo mikono yako imezifanya.

6143:6 Kut 9:29; Ay 11:13; Za 28:2Nanyoosha mikono yangu kwako,

nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame.

7143:7 Za 69:17; 142:3; 22:24; 27:9; 30:7Ee Bwana, unijibu haraka,

roho yangu inazimia.

Usinifiche uso wako,

ama sivyo nitafanana na wale washukao shimoni.

8143:8 Kut 33:13; Ay 34:32; Za 6:4; 90:14; 27:11; 32:8; 25:1-2; 86:4Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma,

kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako.

Nionyeshe njia nitakayoiendea,

kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu.

9143:9 Za 140:1; 18:17; 31:15Ee Bwana, uniokoe na adui zangu,

kwa kuwa nimejificha kwako.

10143:10 Za 119:12; 31:14; 25:4-5; 26:11; Neh 9:20; Yn 14:26; Rum 5:5; Efe 4:30; Gal 5:22, 23Nifundishe kufanya mapenzi yako,

kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu,

Roho wako mwema na aniongoze

katika nchi tambarare.

11143:11 Za 25:11; 41:2; 31:1; 71:2Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu,

kwa haki yako nitoe katika taabu.

12143:12 Za 8:2; 54:5; 116:16Kwa upendo wako usiokoma,

nyamazisha adui zangu;

waangamize watesi wangu wote,

kwa kuwa mimi ni mtumishi wako.