Zaburi 142 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 142:1-7

Zaburi 142

Maombi Ya Kuokolewa Dhidi Ya Watesi

Utenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Maombi.

1142:1 1Fal 8:52; Za 3:4; 30:8Namlilia Bwana kwa sauti,

nainua sauti yangu kwa Bwana anihurumie.

2142:2 Za 64:1; 50:15Namimina malalamiko yangu mbele zake,

mbele zake naeleza shida zangu.

3142:3 Za 6:2; 77:3; 84:2; 88:4; 143:4, 7; Yer 4:18; Mao 1:22Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu,

wewe ndiwe unajua njia zangu.

Katika njia ninayopita

watu wameniwekea mtego.

4142:4 Yer 25:35; 30:17Tazama kuume kwangu na uone,

hakuna hata mmoja anayejihusisha nami.

Sina kimbilio,

hakuna anayejali maisha yangu.

5142:5 Za 16:5; 27:13; 46:1; Kum 32:9; Ay 28:13; Mao 3:24Ee Bwana, nakulilia wewe,

nasema, “Wewe ni kimbilio langu,

fungu langu katika nchi ya walio hai.”

6142:6 Za 17:1; 79:8; 25:20; Yer 31:11Sikiliza kilio changu,

kwa sababu mimi ni mhitaji sana;

niokoe na wale wanaonifuatilia,

kwa kuwa wamenizidi nguvu.

7142:7 Za 66:11; 7:17; 9:2; 2Nya 6:41Nifungue kutoka kifungo changu,

ili niweze kulisifu jina lako.

Ndipo wenye haki watanizunguka,

kwa sababu ya wema wako kwangu.