Zaburi 141 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 141:1-10

Zaburi 141

Maombi Ya Kuhifadhiwa Dhidi Ya Uovu

Zaburi ya Daudi.

1141:1 Za 22:19; 4:1; 5:1-2; 27:7; 143:1Ee Bwana, ninakuita wewe, uje kwangu hima.

Sikia sauti yangu ninapokuita.

2141:2 Lk 1:9; Ufu 5:8; 8:3; Za 28:2; 63:4; 1Tim 2:8; Kut 29:39, 41; 30:8; Efe 5:2Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba;

kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni.

3141:3 Za 34:13; 12:2; Yak 1:26; 3:8Ee Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu,

weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.

4141:4 Yos 24:23; Za 106:29; Mit 23:1-3Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya,

nisije nikashiriki katika matendo maovu

pamoja na watu watendao mabaya,

wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa.

5141:5 Mit 9:8; 19:25; 25:12; Mhu 7:5; Kut 29:7; Za 23:5Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma;

na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu.

Kichwa changu hakitalikataa.

Hata hivyo, maombi yangu daima

ni kinyume cha watenda mabaya,

6141:6 2Nya 25:12watawala wao watatupwa chini

kutoka kwenye majabali,

waovu watajifunza kwamba maneno yangu

yalikuwa kweli.

7141:7 Za 129:3; Hes 16:32-33; 16:30; 2Kor 1:9Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi,

ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.”

8141:8 Za 123:2; 2:12; 11:1Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mwenyezi,

ndani yako nimekimbilia, usiniache nife.

9141:9 Za 140:4; 64:5; 38:12Niepushe na mitego waliyonitegea,

kutokana na mitego iliyotegwa na watenda mabaya.

10141:10 Za 7:15; 35:8; 57:6; 124:7Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe,

wakati mimi ninapita salama.