Zaburi 140 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 140:1-13

Zaburi 140

Kuomba Ulinzi Wa Mungu

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1140:1 Za 17:13; 25:20; 59:2; 71:4; 142:6; 143:9; 86:14Ee Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu;

nilinde na watu wenye jeuri,

2140:2 Mit 6:14; 16:27; Isa 59:4; Hos 7:15; Za 36:4; 52:2; 68:30ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao,

na kuchochea vita siku zote.

3140:3 Za 57:4; 58:4; Rum 3:13; Yak 3:8Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka,

sumu ya nyoka iko midomoni mwao.

4140:4 Za 141:9; 36:11Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu;

nilinde na watu wenye jeuri

wanaopanga kunikwaza miguu yangu.

5140:5 Ay 34:30; Za 31:4; 38:12; 119:110; Ay 18:8; 18:9Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa,

wametandaza kamba za wavu wao,

wametega mitego kwenye njia yangu.

6140:6 Za 16:2; 28:2, 6Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.”

Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia.

7Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu,

unikingaye kichwa changu siku ya vita:

8140:8 Za 10:2-3; 66:7; Ay 5:12-13Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao,

usiache mipango yao ikafanikiwa,

wasije wakajisifu.

9140:9 Mit 18:7Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe

na shida zinazosababishwa na midomo yao.

10140:10 Za 11:6; 21:9; Mt 3:10; Lk 12:40; Ufu 20:15Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie!

Na watupwe motoni,

katika mashimo ya matope,

wasiinuke tena kamwe.

11140:11 Za 34:21Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi;

maafa na yawawinde watu wenye jeuri.

12140:12 1Fal 8:45; Za 35:10; 82:3; 109:31Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki,

na kuitegemeza njia ya mhitaji.

13140:13 Za 138:2; 11:7; 16:11Hakika wenye haki watalisifu jina lako,

na waadilifu wataishi mbele zako.