Zaburi 14 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 14:1-7

Zaburi 14

Uovu Wa Wanadamu

(Zaburi 53)

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

114:1 Za 10:4; Mwa 6:12; Rum 3:10; Mit 1:7, 22Mpumbavu anasema moyoni mwake,

“Hakuna Mungu.”

Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa;

hakuna hata mmoja atendaye mema.

214:2 Ay 41:34; Za 32:6; 85:11; 102:19; Ezr 6:21; Mao 3:50Bwana anawachungulia wanadamu chini

kutoka mbinguni

aone kama wako wenye akili,

wowote wanaomtafuta Mungu.

314:3 1Sam 8:3; 2Pet 2:7; 1Tim 5:15; 1Fal 8:46; Za 143:2; Mhu 7:20; Rum 3:10-12Wote wamepotoka,

wameharibika wote pamoja,

hakuna atendaye mema.

Naam, hakuna hata mmoja!

414:4 Za 17:2; 82:5; 79:6; Mik 3:3; Isa 64:7; 65:1; Yer 4:22; 10:25; Hos 7:7Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza:

wale ambao huwala watu wangu

kama watu walavyo mkate,

hao ambao hawamwiti Bwana?

5Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu,

maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.

614:6 2Sam 22:3Ninyi watenda mabaya mnakwamisha mipango ya maskini,

bali Bwana ndiye kimbilio lao.

714:7 Za 2:6; Yer 48:47; Kum 30:3Laiti wokovu wa Israeli

ungalikuja kutoka Sayuni!

Wakati Bwana arejeshapo

wafungwa wa watu wake,

Yakobo na ashangilie,

Israeli na afurahi!