Zaburi 137
Maombolezo Ya Israeli Uhamishoni
1137:1 Eze 1:1; Dan 8:2Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza
tulipokumbuka Sayuni.
2137:2 Isa 24:8; Ay 30:9; 30:31; Ufu 18:22; Amo 6:5; 8:10; Mao 1:5; 5:15; Za 79:1-4; 80:6; Eze 16:57; 22:4; 34:29; 26:13Kwenye miti ya huko
tulitundika vinubi vyetu,
3137:3 Mao 1:5; Za 79:1-4; 80:6; Eze 16:57; 22:4; 34:29; Ay 30:9kwa maana huko hao waliotuteka
walitaka tuwaimbie nyimbo,
watesi wetu walidai nyimbo za furaha;
walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!”
4137:4 Neh 12:46Tutaimbaje nyimbo za Bwana,
tukiwa nchi ya kigeni?
5137:5 Isa 2:3; 56:7; 65:11; 66:20Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu,
basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.
6137:6 Za 22:15; Neh 2:3; Yer 51:50; Kum 4:29; Eze 3:26; 6:9Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu
kama sitakukumbuka wewe,
kama nisipokufikiri Yerusalemu
kuwa furaha yangu kubwa.
7137:7 Mwa 25:30; 2Nya 28:17; Za 74:8; 83:6; Mao 1:10; 4:21-22; 2Fal 25:1-10Kumbuka, Ee Bwana, walichokifanya Waedomu,
siku ile Yerusalemu ilipoanguka.
Walisema, “Bomoa, Bomoa
mpaka kwenye misingi yake!”
8137:8 Yer 25:12, 26; 50:1; Isa 13:1, 19; 47:1-15Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa,
heri yeye atakayekulipiza wewe
kwa yale uliyotutenda sisi:
9137:9 2Fal 8:12; Isa 13:16; Lk 19:44yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga
na kuwaponda juu ya miamba.