Zaburi 131 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 131:1-3

Zaburi 131

Kumtegemea Mungu Kwa Unyenyekevu

Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1131:1 Isa 2:12; Yer 45:5; Rum 12:16; 2Sam 22:28; Ay 41:34; 5:9; Za 101:5; 139:6Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana,

macho yangu hayajivuni;

sijishughulishi na mambo makuu kunizidi

wala mambo ya ajabu mno kwangu.

2131:2 Za 116:7; Mit 18:3; Mt 18:3; 1Kor 13:11; 14:20Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu;

kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake,

kama mtoto aliyeachishwa kunyonya

ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu.

3131:3 Za 25:5; 130:7; 113:2; 119:43Ee Israeli, mtumaini Bwana

tangu sasa na hata milele.