Zaburi 126 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 126:1-6

Zaburi 126

Kurejezwa Kutoka Utumwani

Wimbo wa kwenda juu.

1126:1 Ezr 1:1-3; Za 85:1; Hos 6:11; Mdo 12:9Bwana alipowarejeza mateka Sayuni,

tulikuwa kama watu walioota ndoto.

2126:2 Mwa 21:6; Ay 8:21; Kum 10:21; Za 65:8; 71:19; Lk 1:49Vinywa vyetu vilijaa kicheko,

ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.

Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,

Bwana amewatendea mambo makuu.”

3126:3 Za 9:2; 16:11; 106:21; Yoe 2:21, 26Bwana ametutendea mambo makuu,

nasi tumejaa furaha.

4126:4 Kum 30:3; Za 107:35; Isa 43:19; 51:3Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa,

kama vijito katika Negebu.

5126:5 Za 16:11; 20:5; 23:6; 6:6; 80:5; Yer 50:4; Gal 6:9; Isa 12:1-3; 35:10; 51:11; 60:15; 61:7; Yer 31:6-7, 12Wapandao kwa machozi

watavuna kwa nyimbo za shangwe.

6Yeye azichukuaye mbegu zake

kwenda kupanda, huku akilia,

atarudi kwa nyimbo za shangwe,

akichukua miganda ya mavuno yake.