Zaburi 124 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 124:1-8

Zaburi 124

Shukrani Kwa Ukombozi Wa Israeli

Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1124:1 Za 129:1; Mwa 15:1; Hes 14:9; Yos 1:5Kama Bwana asingalikuwa upande wetu;

Israeli na aseme sasa:

2kama Bwana asingalikuwa upande wetu,

wakati watu walipotushambulia,

3124:3 Za 35:25; Mit 1:12; Yer 51:34wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu,

wangalitumeza tungali hai,

4124:4 Za 88:17; 18:4mafuriko yangalitugharikisha,

maji mengi yangalitufunika,

5maji yaendayo kasi

yangalituchukua.

6Bwana asifiwe,

yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.

7124:7 Za 91:3; 25:15Tumeponyoka kama ndege

kutoka mtego wa mwindaji;

mtego umevunjika,

nasi tukaokoka.

8124:8 1Sam 17:45; Mwa 1:1; Za 115:15; 121:2; 134:3; Kut 18:4; Mit 18:10; Isa 50:10Msaada wetu ni katika jina la Bwana,

Muumba wa mbingu na dunia.