Zaburi 122 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 122:1-9

Zaburi 122

Sifa Kwa Yerusalemu

Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1122:1 Isa 49:10; Yer 31:6; Zek 8:21Nilishangilia pamoja na wale walioniambia,

“Twende nyumbani ya Bwana.”

2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama

malangoni mwako.

3122:3 2Sam 5:9; Efe 2:21Yerusalemu imejengwa vyema kama mji

ambao umeshikamanishwa pamoja.

4122:4 Kum 16:16; Kut 16:34Huko ndiko makabila hukwea,

makabila ya Bwana,

kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo

waliopewa Israeli.

5Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa,

viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.

6122:6 Za 26:8; Isa 62:6; Yer 51:50Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu:

“Wote wakupendao na wawe salama.

7122:7 1Sam 25:6; Za 48:3Amani na iwepo ndani ya kuta zako

na usalama ndani ya ngome zako.”

8Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki,

nitasema, “Amani iwe ndani yako.”

9122:9 Za 128:5Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu,

nitatafuta mafanikio yako.