Zaburi 121 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 121:1-8

Zaburi 121

Bwana Mlinzi Wetu

Wimbo wa kwenda juu.

1Nayainua macho yangu nitazame vilima,

msaada wangu utatoka wapi?

2121:2 Mwa 1:1; Za 104:5Msaada wangu hutoka kwa Bwana,

Muumba wa mbingu na dunia.

3121:3 1Sam 2:9; Isa 27:3Hatauacha mguu wako uteleze,

yeye akulindaye hatasinzia,

4121:4 Za 127:1hakika, yeye alindaye Israeli

hatasinzia wala hatalala usingizi.

5121:5 Za 1:6Bwana anakulinda,

Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume,

6121:6 Isa 49:10jua halitakudhuru mchana,

wala mwezi wakati wa usiku.

7121:7 Za 9:9, 10; 91:9, 10; Ay 5:19; Mit 12:21Bwana atakukinga na madhara yote,

atayalinda maisha yako,

8121:8 Kum 28:6; Mit 2:8Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka,

tangu sasa na hata milele.