Zaburi 119 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 119:1-176

Zaburi 119119:0 Zaburi hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi 22 za alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T).

Sifa Za Sheria Ya Bwana

Kujifunza Sheria Ya Bwana

1119:1 Mwa 17:1; Za 1:2; 128:1; Kum 18:13; Mit 11:20Heri wale walio waadilifu katika njia zao,

wanaoenenda katika sheria ya Bwana.

2119:2 Za 40:16; 112:1; 119:146; Isa 56:2; Kum 10:12; Mit 9:7; 1Nya 16:11Heri wale wanaozishika shuhuda zake,

wamtafutao kwa moyo wao wote.

3119:3 Za 59:4; 128:1; Yn 3:9; 5:18; Yer 6:16; 7:23; Rum 7:16, 17Wasiofanya lolote lililo baya,

wanaoenenda katika njia zake.

4119:4 Za 103:18; 119:56; Kum 6:17Umetoa maagizo yako

ili tuyatii kwa ukamilifu.

5119:5 Law 19:37; Yer 31:33; 2Kor 3:5; Rum 7:22, 23Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara

katika kuyatii maagizo yako!

6119:6 Za 119:46, 80, 117; Ay 22:26; 1Yn 2:28Hivyo mimi sitaaibishwa

ninapozingatia amri zako zote.

7119:7 Kum 4:8119:7 Za 90:13; 103:13; 119:47Nitakusifu kwa moyo mnyofu

ninapojifunza sheria zako za haki.

8119:8 Za 38:21Nitayatii maagizo yako;

usiniache kabisa.

Kutii Sheria Ya Bwana

9119:9 Za 119:65, 169; 39:1; Mit 1:4, 10Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?

Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

10119:10 Za 119:21, 118; 9:1; 2Nya 15:15Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,

usiniache niende mbali na amri zako.

11119:11 Isa 63:13; Mit 3:23; Za 119:133, 165; 18:22-23; Kum 6:6; Lk 2:19; Ay 22:22Nimelificha neno lako moyoni mwangu

ili nisikutende dhambi.

12119:12 Isa 63:13; Lk 2:19Sifa ni zako, Ee Bwana,

nifundishe maagizo yako.

13119:13 Za 119:72Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote

zinazotoka katika kinywa chako.

14119:14 Za 119:111Ninafurahia kufuata sheria zako

kama mtu afurahiaye mali nyingi.

15119:15 Za 119:97, 148; 1:2Ninatafakari maagizo yako

na kuziangalia njia zako.

16119:16 Za 112:1Ninafurahia maagizo yako,

wala sitalipuuza neno lako.

Furaha Katika Sheria Ya Bwana

17119:17 Za 13:6; 116:7; 119:67; 103:20Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi;

nitalitii neno lako.

18Yafungue macho yangu nipate kuona

mambo ya ajabu katika sheria yako.

19119:19 Mwa 23:4; Ebr 11:13Mimi ni mgeni duniani,

usinifiche amri zako.

20119:20 Za 84:2; 119:131; 42:2; 63:1; Isa 26:9Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa

juu ya sheria zako wakati wote.

21119:21 Za 119:10, 51; 5:5; Ay 30:1; Yer 20:7; 50:32; Kum 27:26; Dan 4:37; Mal 3:15Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa

waendao mbali na amri zako.

22119:22 Za 39:8; 119:2Niondolee dharau na dhihaka,

kwa kuwa ninazishika sheria zako.

23Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia,

mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako.

24Sheria zako ni furaha yangu,

nazo ni washauri wangu.

Kuamua Kuitii Sheria Ya Bwana

25119:25 Za 44:25; 143:11; 119:9, 50, 107Nimelazwa chini mavumbini,

yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

26119:26 Za 25:4; 27:11; 86:11; 1Fal 8:36Nilikueleza njia zangu ukanijibu,

nifundishe sheria zako.

27119:27 Za 105:2; 145:5Nijulishe mafundisho ya mausia yako,

nami nitatafakari maajabu yako.

28119:28 Za 119:9; 116:3; 18:1; 6:7; Yer 45:3; Isa 51:11; 40:29; 41:10Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni,

uniimarishe sawasawa na neno lako.

29119:29 Za 26:4; Hes 6:25; Mit 30:8; Ebr 8:10Niepushe na njia za udanganyifu,

kwa neema unifundishe sheria zako.

30119:30 Yos 24:22; Za 26:3; 108:1Nimechagua njia ya kweli,

nimekaza moyo wangu katika sheria zako.

31119:31 Kum 10:20Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana,

usiniache niaibishwe.

32119:32 1Fal 4:29; Isa 60:5; 2Kor 6:11Nakimbilia katika njia ya maagizo yako,

kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.

Maombi Ili Kupata Ufahamu Wa Sheria

33119:33 Za 119:12Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako,

nami nitayashika mpaka mwisho.

34119:34 Za 119:27, 69, 73, 144, 169; Mit 2:6; Ay 32:8; Yak 1:5; Kum 6:25; Dan 2:21Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako

na kuitii kwa moyo wangu wote.

35119:35 Za 119:32; 1:2; 25:4, 5Niongoze kwenye njia ya amri zako,

kwa kuwa huko napata furaha.

36119:36 Yos 24:23; Ebr 13:5; Mk 7:21; 12:15; Eze 33:31; 1Tim 6:10Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako,

na siyo kwenye mambo ya ubinafsi.

37119:37 Za 119:9, 25; 71:20; Ay 31:1Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa,

uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

38119:38 Hes 23:19; 2Sam 7:25Mtimizie mtumishi wako ahadi yako,

ili upate kuogopwa.

39119:39 Za 119:22; 69:9; 89:51; Isa 25:8; 51:7; 54:4Niondolee aibu ninayoiogopa,

kwa kuwa sheria zako ni njema.

40119:40 Za 119:20, 25, 149, 154Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako!

Hifadhi maisha yangu katika haki yako.

Kuitumainia Sheria Ya Bwana

41119:41 Za 6:4; 119:76, 116, 154, 170Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie,

wokovu wako sawasawa na ahadi yako,

42119:42 Mit 27:11; Za 42:10ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki,

kwa kuwa ninalitumainia neno lako.

43119:43 Za 119:74, 81, 114, 147; 1Fal 17:24Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu,

kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako.

44119:44 Za 119:33, 34, 55; Kum 6:25Nitaitii amri yako daima,

naam, milele na milele.

45119:45 Za 119:94, 155; Yn 8:32, 36; Rum 8:2Nitatembea nikiwa huru,

kwa kuwa nimejifunza mausia yako.

46119:46 Mt 10:18; Mdo 26:1, 2; Za 119:6Nitasema sheria zako mbele za wafalme

wala sitaaibishwa,

47119:47 Za 119:77, 97, 127, 143, 159, 163, 165kwa kuwa ninazifurahia amri zako

kwa sababu ninazipenda.

48119:48 Mwa 24:63Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu,

nami ninatafakari juu ya maagizo yako.

Matumaini Katika Sheria Ya Bwana

49119:49 Za 119:9, 43Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako,

kwa sababu umenipa tumaini.

50119:50 Za 119:25; 27:13; Yer 15:16; Rum 5:3-5; Ebr 6:17-19Faraja yangu katika mateso yangu ni hii:

Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.

51119:51 Za 119:21; Ay 16:10; 17:2; 23:11; Yer 20:7Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka,

hata hivyo sitaiacha sheria yako.

52119:52 Za 103:18Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani,

nazo zinanifariji.

53119:53 Kut 32:19; 33:4; Za 89:30; Ezr 9:3Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu,

ambao wameacha sheria yako.

54119:54 Za 119:172; 101:1; 138:5Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu

popote ninapoishi.

55119:55 Za 119:44, 62, 72; 1:2; 42:8; 63:6; 77:2; Isa 26:9; Mdo 16:25Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako,

nami nitatii sheria yako.

56119:56 Za 119:4, 100, 134; Hes 15:40Hili limekuwa zoezi langu:

nami ninayatii mausia yako.

Kujitolea Katika Sheria Ya Bwana

57119:57 Kum 32:9; Yer 51:19; Za 119:17, 67, 101; Mao 3:24Ee Bwana, wewe ni fungu langu,

nimeahidi kuyatii maneno yako.

58119:58 Kum 4:29; Ezr 9:8; 1Nya 16:11; Za 34:4; 119:41; Mwa 43:29Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote,

nihurumie sawasawa na ahadi yako.

59119:59 Yoe 2:13; Lk 15:17; Yos 24:14, 15Nimezifikiri njia zangu

na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako.

60119:60 Za 119:115Nitafanya haraka bila kuchelewa

kuzitii amri zako.

61119:61 Za 119:83, 109, 153, 176Hata waovu wanifunge kwa kamba,

sitasahau sheria yako.

62119:62 Za 119:55; 119:7; Mdo 16:25Usiku wa manane ninaamka kukushukuru

kwa sababu ya sheria zako za haki.

63119:63 Za 15:4; 101:6, 7; 103:11; 119:56; 111:10Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao,

kwa wote wanaofuata mausia yako.

64119:64 Za 33:5; 119:12, 108Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako,

nifundishe maagizo yako.

Thamani Ya Sheria Ya Bwana

65119:65 Isa 50:2; 59:1; Za 119:9, 17; 125:4; Mik 2:7Mtendee wema mtumishi wako

Ee Bwana, sawasawa na neno lako.

66119:66 Za 51:6Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri,

kwa kuwa ninaamini amri zako.

67119:67 Za 116:10; 95:10; 119:17; Ebr 12:11; Yer 8:4; 31:18; Kum 32:15; Ufu 3:19Kabla sijapata shida nilipotea njia,

lakini sasa ninalitii neno lako.

68119:68 Za 100:5; 106:1; 107:1; 135:3; Kut 18:20; 34:6; Mt 19:17Wewe ni mwema, unalotenda ni jema,

nifundishe maagizo yako.

69119:69 Ay 13:4; Za 109:2Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo,

nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote.

70119:70 Mdo 28:27; Za 17:10; Isa 29:13Mioyo yao ni katili na migumu,

bali mimi napendezwa na sheria yako.

71119:71 Za 119:67, 75; Ebr 12:10Ilikuwa vyema mimi kupata shida

ili nipate kujifunza maagizo yako.

72119:72 Ay 28:17; Za 19:10; Mt 8:10Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu

kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.

Haki Ya Sheria Ya Bwana

73119:73 Mwa 1:27; Ay 4:17; 10:8; Za 139:13-16; 100:3; 138:8Mikono yako ilinifanya na kuniumba,

nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.

74119:74 Za 34:2; 119:9; 130:5Wakuchao wafurahie wanaponiona,

kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.

75119:75 Za 89:30, 31; 119:7, 138, 172; Ebr 12:5-11Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki,

katika uaminifu wako umeniadhibu.

76119:76 Za 6:4; 119:41Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu,

sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.

77Huruma yako na inijie ili nipate kuishi,

kwa kuwa naifurahia sheria yako.

78119:78 Za 119:51; 35:19; 119:86, 161; 25:3; Yer 50:32Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu,

lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako.

79119:79 Za 119:27, 125Wale wakuchao na wanigeukie mimi,

hao ambao wanazielewa sheria zako.

80119:80 Za 119:1; 119:6; 1Fal 8:61; Mwa 26:5Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako,

ili nisiaibishwe.

Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa

81119:81 Za 119:20, 43, 123; 84:2; 73:26Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako,

lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.

82119:82 Mao 2:11; Za 6:7; 69:3; 119:41, 123Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako;

ninasema, “Utanifajiri lini?”

83119:83 Za 119:61; 119:84; Ay 30:30; Ufu 6:10; Yer 12:3; 15:15; 20:11; Za 39:4; 6:3; 119:51; 7:6Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi,

bado sijasahau maagizo yako.

84Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini?

Ni lini utawaadhibu washtaki wangu?

85119:85 Za 35:7; 119:51; 57:6; Yer 18:20, 22Wenye majivuno wananichimbia mashimo,

kinyume na sheria yako.

86119:86 Za 109:26; 7:1-5; 35:19; 119:78, 138Amri zako zote ni za kuaminika;

unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu.

87119:87 Isa 1:4, 28; 59:13; 58:2; Za 119:150Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia,

lakini sijaacha mausia yako.

88119:88 Za 41:2; 119:2, 100, 124, 129, 134, 168; 51:1; 109:26Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako,

nami nitatii sheria za kinywa chako.

Imani Katika Sheria Ya Bwana

89119:89 Za 119:111, 144; 111:8; Isa 51:6; Mt 5:18; 1Pet 1:25Ee Bwana, neno lako ni la milele,

linasimama imara mbinguni.

90119:90 Za 36:5; 45:17; 148:6; Ay 8:19Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote,

umeiumba dunia, nayo inadumu.

91119:91 Yer 33:25; 31:35; Za 148:6; 104:2-4; Mwa 8:22Sheria zako zinadumu hadi leo,

kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.

92119:92 Za 37:4, 5; 112:1; 119:50, 67; Rum 15:4Kama nisingefurahia sheria yako,

ningeangamia katika taabu zangu.

93119:93 Za 119:83; 103:5Sitasahau mausia yako kamwe,

kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.

94119:94 Za 119:45, 146; 54:1; 116:4; Yer 17:14; 31:18; 42:11; Hos 2:7, 16Uniokoe, kwa maana mimi ni wako,

kwa kuwa nimetafuta mausia yako.

95119:95 Za 69:4; 119:99Waovu wanangojea kuniangamiza,

bali mimi ninatafakari sheria zako.

96119:96 Za 19:7; Isa 40:8; Mt 5:18Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo,

lakini amri zako hazina mpaka.

Kuipenda Sheria Ya Bwana

97119:97 Za 1:2; 119:15, 47Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.

Ninaitafakari mchana kutwa.

98119:98 2Tim 3:17; Kum 4:6, 8; 19:7; Isa 48:17Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu,

kwa kuwa nimezishika daima.

99119:99 2Tim 3:15; Za 119:15Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote,

kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.

100119:100 Ay 12:12; 32:7; Za 119:56; Kum 6:17Nina ufahamu zaidi kuliko wazee,

kwa kuwa ninayatii mausia yako.

101119:101 Mit 1:15; 2Kor 7:1; Za 119:57Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya,

ili niweze kutii neno lako.

102119:102 Kum 17:20; 4:5Sijaziacha sheria zako,

kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe.

103119:103 Mit 24:13, 14; 8:11; Za 19:10Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu,

matamu kuliko asali katika kinywa changu!

104119:104 Za 111:10; 119:7Ninapata ufahamu kutoka mausia yako,

kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.

Nuru Kutoka Kwenye Sheria Ya Bwana

105119:105 Mit 6:23; 20:27; 2Pet 1:19; Za 119:130Neno lako ni taa ya miguu yangu

na mwanga katika njia yangu.

106119:106 Neh 10:29; Za 119:7Nimeapa na nimethibitisha,

kwamba nitafuata sheria zako za haki.

107119:107 Za 119:25Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana,

sawasawa na neno lako.

108119:108 Za 51:15; 109:30; 63:5; 119:64; 71:8; Ebr 13:15; Hos 14:2Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu,

nifundishe sheria zako.

109119:109 Amu 12:3; Za 119:61; Ay 13:14Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote,

sitasahau sheria yako.

110119:110 Za 25:15; 64:5; 119:10; Isa 8:14; Amo 3:5Waovu wamenitegea mtego,

lakini sijayakiuka maagizo yako.

111119:111 Kum 33:4; Za 119:14, 162Sheria zako ni urithi wangu milele,

naam ni furaha ya moyo wangu.

112119:112 Za 108:1; 119:33Nimekusudia moyoni mwangu

kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.

Usalama Ndani Ya Sheria Ya Bwana

113119:113 1Fal 18:21; Yak 1:8; 4:8; Za 119:47Ninachukia watu wa nia mbili,

lakini ninapenda sheria yako.

114119:114 Za 18:2; 119:43; 32:7; Mwa 15:1Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu,

nimeweka tumaini langu katika neno lako.

115119:115 Za 6:8; Mt 7:23Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya,

ili niweze kushika amri za Mungu wangu!

116119:116 Za 18:35; 41:3; 55:22; 119:41; Isa 46:4; Rum 5:5; 9:33Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi;

usiache matumaini yangu yakavunjwa.

117119:117 Isa 41:10; 46:4; Za 34:4; 119:6; 71:6; Yn 10:28; Rum 14:4Nitegemeze, nami nitaokolewa,

nami daima nitayaheshimu maagizo yako.

118119:118 Za 119:10Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako,

kwa maana udanganyifu wao ni bure.

119119:119 Isa 1:22, 25; Eze 18:19; Za 119:47Waovu wa nchi unawatupa kama takataka,

kwa hivyo nazipenda sheria zako.

120119:120 Ay 4:14Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe,

ninaziogopa sheria zako.

Kuitii Sheria Ya Bwana

121119:121 2Sam 8:15; Ay 27:6Nimetenda yaliyo haki na sawa,

usiniache mikononi mwa watesi wangu.

122119:122 Ay 17:3Mhakikishie mtumishi wako usalama,

usiache wenye kiburi wanionee.

123119:123 Isa 38:14; Za 119:81, 82Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako,

na kuitazamia ahadi yako ya kweli.

124119:124 Za 119:12, 88; 25:7Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako

na unifundishe maagizo yako.

125119:125 Za 116:16; 119:79Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu

ili niweze kuelewa sheria zako.

126119:126 Hes 15:31Ee Bwana, wakati wako wa kutenda umewadia,

kwa kuwa sheria yako inavunjwa.

127119:127 Efe 3:8; Za 19:10; 119:47; Ay 3:21; Mit 3:13, 18; 8:11Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu,

naam, zaidi ya dhahabu safi,

128119:128 Za 19:8; 31:6; 119:104, 163; Mit 13:5na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili,

nachukia kila njia potovu.

Shauku Ya Kuitii Sheria Ya Bwana

129119:129 Za 119:18, 22, 88Sheria zako ni za ajabu,

hivyo ninazitii.

130119:130 Za 119:105; 19:7, 10; Mit 1:4; 2Pet 1:19Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru,

kunampa mjinga ufahamu.

131119:131 Za 42:1; 119:20Nimefungua kinywa changu na kuhema,

nikitamani amri zako.

132119:132 2Sam 24:14; Kut 4:31; Za 6:4; 9:13; 5:11; 106:4; 1Sam 1:11Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote

wale wanaolipenda jina lako.

133119:133 Kum 6:12; Za 119:9, 11, 122; Rum 6:16Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako,

usiache dhambi yoyote initawale.

134119:134 Lk 1:74; Za 119:56, 88, 122Niokoe na uonevu wa wanadamu,

ili niweze kutii mausia yako.

135119:135 Hes 6:25; Za 4:6; 80:3; 4:6; 119:12Mwangazie mtumishi wako uso wako

na unifundishe amri zako.

136119:136 Yer 9:1; 9:1, 18; 13:17; 14:17; Mao 1:16; 3:48; Isa 22:4; 42:24; Eze 9:4; Za 6:6; 119:158; 106:25Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu,

kwa kuwa sheria yako haifuatwi.

Haki Ya Sheria Ya Bwana

137119:137 Kut 9:27; Ezr 9:15; Neh 9:13, 33; Yer 12:1; Dan 9:7Ee Bwana, wewe ni mwenye haki,

sheria zako ni sahihi.

138119:138 Za 119:75, 86; 19:7Sheria ulizoziweka ni za haki,

ni za kuaminika kikamilifu.

139119:139 Za 69:9; Yn 2:17Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu

wanayapuuza maneno yako.

140119:140 Yos 23:14; Za 12:6; 119:47Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu,

mtumishi wako anazipenda.

141119:141 Za 22:6; 119:61, 134; Mit 15:16; Amo 7:2; Lk 6:20; 2Kor 8:9; Yak 2:5Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa,

sisahau mausia yako.

142119:142 Za 119:151, 160; 19:7, 9; Yn 17:17; Efe 1:3Haki yako ni ya milele,

na sheria yako ni kweli.

143119:143 Za 119:24, 47Shida na dhiki zimenipata,

lakini amri zako ni furaha yangu.

144119:144 Za 119:34Sheria zako ni sahihi milele,

hunipa ufahamu ili nipate kuishi.

Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa

145119:145 Za 119:10, 22, 55Ee Bwana, ninakuita kwa moyo wangu wote,

nami nitayatii maagizo yako.

146119:146 Za 119:94Ninakuita; niokoe

nami nitazishika sheria zako.

147119:147 Za 3:3; 57:8; 108:2Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada;

nimeweka tumaini langu katika neno lako.

148119:148 Za 63:6; 63:1, 6Sikufumba macho yangu usiku kucha,

ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.

149119:149 Za 27:7; 124; 119:40Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako,

Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako.

150119:150 Za 37:7Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami,

lakini wako mbali na sheria yako.

151119:151 Flp 4:5; Za 34:18; 119:142; 145:18Ee Bwana, hata hivyo wewe u karibu,

na amri zako zote ni za kweli.

152119:152 Za 119:7, 73, 89; 111:8; Lk 21:33Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako

kwamba umezithibitisha ili zidumu milele.

Maombi Kwa Ajili Ya Msaada

153119:153 Za 13:3; 3:7; 44:17; Mao 5:1Yaangalie mateso yangu, uniokoe,

kwa kuwa sijasahau sheria yako.

154119:154 Za 119:24, 41; 35:1; 1Sam 24:15; Yer 50:34; Mik 7:9Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe,

uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako.

155119:155 Za 119:94, 118; Ay 5:4Wokovu uko mbali na waovu,

kwa kuwa hawatafuti maagizo yako.

156119:156 Neh 9:27; Yak 5:11; Za 119:25, 149Ee Bwana, huruma zako ni kuu,

uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako.

157119:157 Za 7:1; 44:18Adui wanaonitesa ni wengi,

lakini mimi sitaziacha sheria zako.

158119:158 Za 119:104, 136; Kut 32:19Ninawatazama wasioamini kwa chuki,

kwa kuwa hawalitii neno lako.

159119:159 Za 119:25; 41:2Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako;

Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako.

160119:160 Za 119:89; 111:8Maneno yako yote ni kweli,

sheria zako zote za haki ni za milele.

Kujiweka Wakfu Kwa Sheria Ya Bwana

161119:161 Za 119:23, 122, 157; 119:120; 1Sam 24:14-15Watawala wamenitesa bila sababu,

lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako.

162119:162 Za 119:25; 41:2Nafurahia ahadi zako

kama mtu aliyepata mateka mengi.

163Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo,

lakini napenda sheria yako.

164119:164 Za 119:111; 1Sam 30:16; Isa 9:3; 53:12Ninakusifu mara saba kwa siku,

kwa ajili ya sheria zako za haki.

165119:165 Za 119:11; 37:11; 37:24; Isa 26:3, 12; 27:5; 32:17; 57:19; 66:12; 1Yn 2:10; Mit 3:2Wanaopenda sheria yako wana amani tele,

wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza.

166119:166 Za 119:81Ee Bwana, ninangojea wokovu wako,

nami ninafuata amri zako,

167119:167 Za 119:47Ninazitii sheria zako,

kwa sababu ninazipenda mno.

168119:168 Za 139:3; Ay 10:4; 23:10; Mit 5:21Nimetii mausia yako na sheria zako,

kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako.

Kuomba Msaada

169119:169 Ay 16:18; Za 119:9, 34Ee Bwana, kilio changu na kifike mbele zako,

nipe ufahamu sawasawa na neno lako.

170119:170 1Fal 8:30; 2Nya 6:24; Za 28:2; 140:6; 143:1; 3:7; 22:20; 59:1; 119:41Maombi yangu na yafike mbele zako,

niokoe sawasawa na ahadi yako.

171119:171 Za 51:15; 63:3; 94:12; Isa 2:3; Mik 4:2Midomo yangu na ibubujike sifa,

kwa kuwa unanifundisha maagizo yako.

172119:172 Za 51:14; 119:7, 75Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako,

kwa kuwa amri zako zote ni za haki.

173119:173 Za 37:24; 73:23; Isa 41:10; Lk 10:42; Yos 24:22; Mit 1:29Mkono wako uwe tayari kunisaidia,

kwa kuwa nimechagua mausia yako.

174119:174 Za 119:16, 24, 166Ee Bwana, ninatamani wokovu wako,

na sheria yako ni furaha yangu.

175119:175 Za 119:116, 159; Isa 55:3Nijalie kuishi ili nipate kukusifu,

na sheria zako zinitegemeze.

176119:176 Za 119:10; 95:10; Yer 50:17; Eze 34:11; Lk 15:4Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea.

Mtafute mtumishi wako,

kwa kuwa sijasahau amri zako.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

诗篇 119:1-176

第119篇

耶和华的律法

1行为正直、遵行耶和华律法的人有福了!

2遵守祂的法度、全心寻求祂的人有福了!

3他们不做不义之事,

只遵行祂的旨意。

4耶和华啊,你已经赐下法则,

为了让我们竭力遵行。

5我渴望坚定地遵从你的律例。

6我重视你的一切命令,

便不致羞愧。

7我学习你公义的法令时,

要存着正直的心来称谢你。

8我要遵守你的律例,

求你不要完全弃绝我。

9青年如何保持纯洁呢?

就是要遵行你的话。

10我全心寻求你,

求你不要让我偏离你的命令。

11我把你的话珍藏在心中,

免得我得罪你。

12耶和华啊,你当受称颂!

求你将你的律例教导我。

13我宣扬你口中所出的一切法令。

14我喜爱你的法度如同人喜爱财富。

15我要默想你的法则,

思想你的旨意。

16我以遵行你的律例为乐,

我不忘记你的话语。

17求你以厚恩待你仆人,

使我能活着,并遵守你的话语。

18求你开我的眼睛,

使我能明白你律法中的奥妙。

19我在世上是过客,

求你不要向我隐藏你的命令。

20我时刻切慕你的法令,

以致心力憔悴。

21你斥责受咒诅、偏离你命令的狂傲人。

22求你除去我所受的羞辱和藐视,

因为我遵从你的法度。

23虽然权贵们坐着毁谤我,

仆人仍要默想你的律例。

24你的法度是我的喜乐,

是我的谋士。

25我的性命几乎坠入尘埃,

求你凭应许保全我性命。

26我陈明自己的行为,

你就回应了我;

求你将你的律例教导我。

27求你使我明白你的法则,

我要默想你的奇妙作为。

28我伤心欲绝,

求你照你的应许使我坚强起来。

29求你使我远离奸诈之路,

开恩将你的律法教导我。

30我已经选择了真理之路,

决心遵行你的法令。

31我持守你的法度,耶和华啊,

求你不要使我蒙羞。

32我竭力遵守你的命令,

因为你拓宽我的悟性。

33耶和华啊,求你将你的律例教导我,

我必遵守到底。

34求你赐我悟性,使我遵守你的律法,

并且全心遵守。

35求你引导我遵行你的命令,

因为这是我喜爱的。

36求你使我的心向往你的法度,

而非不义之财。

37求你使我的眼目远离虚空之事,

按你的旨意保全我性命。

38求你实现你给仆人的应许,

就是你给敬畏你之人的应许。

39求你除去我所害怕的羞辱,

因为你的法令是美善的。

40我渴望遵行你的法则,

求你按你的公义保全我性命。

41耶和华啊!

愿你的慈爱临到我,

愿你的拯救临到我,

正如你的应许,

42好叫我能应对嘲笑我的人,

因为我信靠你的话。

43断不要从我口中拿走真理之言,

因为你的法令是我的盼望。

44我要持守你的律法,

直到永永远远。

45我要自由地生活,

因为我寻求你的法则。

46我要在君王面前讲论你的法度,

我不以此为耻。

47我以遵行你的命令为乐,

我喜爱你的命令。

48我尊崇你的命令,

我喜爱你的命令,

我要默想你的律例。

49求你顾念你对仆人的应许,

你的话带给我盼望。

50你的应许保全我性命,

是我患难中的安慰。

51狂傲人肆意嘲讽我,

但我仍然没有偏离你的律法。

52耶和华啊,

我牢记你古时赐下的法令,

你的法令是我的安慰。

53我见恶人丢弃你的律法,

就怒火中烧。

54我在世上寄居,

你的律例就是我的诗歌。

55耶和华啊,我在夜间思想你的名,

我要遵守你的律法。

56我向来遵行你的法则。

57耶和华啊,你是我的福分!

我决心遵行你的话语。

58我一心求你施恩,

求你照着你的应许恩待我。

59我思想自己走过的路,

就移步归向你的法度。

60我毫不迟疑地遵守你的命令。

61虽然恶人用绳索捆绑我,

我仍不忘记你的律法。

62因为你公义的法令,

我半夜起来称谢你。

63我与所有敬畏你、遵守你法则的人为友。

64耶和华啊,你的慈爱充满大地,

求你将你的律例教导我。

65耶和华啊,

你信守诺言,善待了仆人。

66求你赐我知识,教我判别是非,

因为我信靠你的命令。

67从前我没有受苦的时候走迷了路,

现在我要遵行你的话。

68你是美善的,

你所行的都是美善的,

求你将你的律例教导我。

69傲慢人毁谤我,

但我一心遵守你的法则。

70他们执迷不悟,

但我喜爱你的律法。

71我受苦对我有益,

使我可以学习你的律例。

72你颁布的律法对我而言比千万金银更宝贵。

73你亲手造我、塑我,

求你赐我悟性来学习你的命令。

74敬畏你的人见我就欢喜,

因为你的话是我的盼望。

75耶和华啊,

我知道你的法令公义,

你是凭信实管教我。

76求你照着你给仆人的应许,

用你的慈爱来安慰我。

77求你怜悯我,使我可以存活,

因为你的律法是我的喜乐。

78愿狂傲人受辱,

因他们诋毁我;

但我要默想你的法则。

79愿敬畏你的人到我这里来,

好明白你的法度。

80愿我能全心遵守你的律例,

使我不致羞愧。

81我的心迫切渴慕你的拯救,

你的话是我的盼望。

82我期盼你的应许实现,

望眼欲穿。

我说:“你何时才安慰我?”

83我形容枯槁,好像烟熏的皮袋,

但我仍然没有忘记你的律例。

84你仆人还要等候多久呢?

你何时才会惩罚那些迫害我的人呢?

85违背你律法的狂傲人挖陷阱害我。

86你的一切命令都可靠,

他们无故地迫害我,

求你帮助我。

87他们几乎置我于死地,

但我仍然没有背弃你的法则。

88求你施慈爱保全我性命,

我好遵守你颁布的法度。

89耶和华啊,你的话立定在天,

永远不变。

90你的信实万代长存;

你奠定大地,它恒久不变。

91天地照你的法令存到今日,

因为万物都是你的仆役。

92我若不以你的律法为乐,

早已死在苦难中了。

93我永不忘记你的法则,

因你借此保全我性命。

94我属于你,求你拯救我,

因为我寻求你的法则。

95恶人伺机害我,

但我仍然思想你的法度。

96我看到万事都有尽头,

唯有你的命令无边无界。

97我多么爱慕你的律法,

终日默想。

98你的命令常在我心中,

它使我比仇敌有智慧。

99我比所有老师更有洞见,

因为我默想你的法度。

100我比长者更明智,

因为我遵守你的法则。

101为了遵行你的话,

我拒绝走恶道。

102我没有偏离你的法令,

因为你教导过我。

103你的话在我上颚何等甘美,

在我口中比蜜还甜。

104我从你的法则中得到智慧,

因此我厌恶一切诡诈之道。

105你的话是我脚前的灯,

是我路上的光。

106我已起誓,我必信守诺言:

我要遵行你公义的法令。

107我饱受痛苦,耶和华啊,

求你照你的话保全我性命。

108耶和华啊,

求你悦纳我由衷的赞美,

将你的法令教导我。

109我的生命时刻面临危险,

但我不会忘记你的律法。

110恶人为我设下网罗,

但我没有偏离你的法则。

111你的法度永远是我的宝贵产业,

是我心中的喜乐。

112我决心遵行你的律例,

一直到底。

113我厌恶心怀二意的人,

我喜爱你的律法。

114你是我的藏身之所,

是我的盾牌,

你的话语是我的盼望。

115你们这些恶人离开我吧,

我要遵行我上帝的命令。

116耶和华啊,

求你按你的应许扶持我,

使我存活,

不要使我的盼望落空。

117求你扶持我,使我得救,

我要时刻关注你的律例。

118你弃绝一切偏离你律例的人,

他们的诡计无法得逞。

119你铲除世上的恶人,

如同除掉渣滓,

因此我喜爱你的法度。

120我因敬畏你而战栗

我惧怕你的法令。

121我做事公平正直,

求你不要把我交给欺压我的人。

122求你保障仆人的福祉,

不要让傲慢的人欺压我。

123我望眼欲穿地期盼你拯救我,

盼望你实现你公义的应许。

124求你凭慈爱待你仆人,

将你的律例教导我。

125我是你的仆人,

求你赐我悟性可以明白你的法度。

126耶和华啊,人们违背你的律法,

是你惩罚他们的时候了。

127所以我爱你的命令胜于爱金子,

胜于爱纯金。

128我遵行你一切的法则,

我憎恨一切恶道。

129你的法度奇妙,

所以我一心遵守。

130你的话语一解明,

就发出亮光,

使愚人得到启迪。

131我张着口气喘吁吁,

因我渴慕你的命令。

132求你眷顾我、怜悯我,

正如你素来恩待爱你名的人。

133求你照你的应许引导我的脚步,

不要让罪恶辖制我。

134求你救我脱离恶人的欺压,

好使我能遵守你的法则。

135求你以容光照耀仆人,

将你的律例教导我。

136我泪流成河,

因为人们不遵行你的律法。

137耶和华啊,你是公义的,

你的法令是公正的。

138你定的法度公义,完全可信。

139我看见仇敌无视你的话语,

就心急如焚。

140你仆人喜爱你的应许,

因为你的应许纯全可靠。

141我虽然卑微、受人藐视,

但我不忘记你的法则。

142你的公义常存,

你的律法是真理。

143我虽然遭遇困苦患难,

但你的命令是我的喜乐。

144你的法度永远公正,

求你赐我悟性,使我存活。

145耶和华啊,我全心呼求你,

求你应允我,

我必遵守你的律例。

146我向你呼求,求你救我,

我必持守你的法度。

147天不亮,

我就起来呼求你的帮助,

你的话语是我的盼望。

148我整夜不睡,默想你的应许。

149耶和华啊,

求你凭你的慈爱垂听我的呼求,

照你的法令保全我性命。

150作恶多端的人逼近了,

他们远离你的律法。

151但耶和华啊,你就在我身边,

你的一切命令都是真理。

152我很早就从你的法度中知道,

你立的法度永远长存。

153求你鉴察我的苦难,搭救我,

因为我没有忘记你的律法。

154求你为我申冤,救赎我,

照你的应许保全我性命。

155恶人不寻求你的律例,

以致得不到拯救。

156耶和华啊,

你有无比的怜悯之心,

求你照你的法令保全我性命。

157迫害我的仇敌众多,

但我却没有偏离你的法度。

158我看见背信之徒就厌恶,

因为他们不遵行你的话。

159耶和华啊,你看我多爱你的法则,

求你施慈爱保全我性命。

160你的话都是真理,

你一切公义的法令永不改变。

161权贵无故迫害我,

但我的心对你的话充满敬畏。

162我喜爱你的应许,

如获至宝。

163我憎恶虚假,

但我喜爱你的律法。

164因你公义的法令,

我要每天七次赞美你。

165喜爱你律法的人大有平安,

什么也不能使他跌倒。

166耶和华啊,我等候你的拯救,

我遵行你的命令。

167我深爱你的法度,一心遵守。

168我遵守你的法则和法度,

你知道我做的每一件事。

169耶和华啊,求你垂听我的呼求,

照你的话赐我悟性。

170求你垂听我的祈求,

照你的应许拯救我。

171愿我的嘴唇涌出赞美,

因你将你的律例教导了我。

172愿我的舌头歌颂你的应许,

因为你一切的命令尽都公义。

173愿你的手随时帮助我,

因为我选择了你的法则。

174耶和华啊,我盼望你的拯救,

你的律法是我的喜乐。

175求你让我存活,我好赞美你,

愿你的法令成为我的帮助。

176我像只迷途的羊,

求你来寻找仆人,

因为我没有忘记你的命令。