Zaburi 118 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 118:1-29

Zaburi 118

Shukrani Kwa Ajili Ya Ushindi

1118:1 1Nya 16:8; Ezr 3:11; 2Nya 7:3; 5:13Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

2118:2 Za 115:9; 106:1; 136:1-26Israeli na aseme sasa:

“Upendo wake wadumu milele.”

3118:3 Kut 30:30; Za 115:10Nyumba ya Aroni na iseme sasa:

“Upendo wake wadumu milele.”

4118:4 Za 115:11Wote wamchao Bwana na waseme sasa:

“Upendo wake wadumu milele.”

5118:5 Za 18:6; 31:7; 77:2; 120:1; 118:21; 34:4; 86:7; 116:1; 138:3Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana,

naye akanijibu kwa kuniweka huru.

6118:6 Kum 31:6; Ebr 13:5; Za 56:5Bwana yuko pamoja nami, sitaogopa.

Mwanadamu anaweza kunitenda nini?

7118:7 Kum 33:29; Ebr 13:6; Za 54:4Bwana yuko pamoja nami,

yeye ni msaidizi wangu.

Nitawatazama adui zangu

wakiwa wameshindwa.

8118:8 Yer 17:5, 7; Za 9:9; 62:8; 5:11; 37:3; 40:4; 108:12; Isa 25:4; 57:13; 2:22; 2Nya 32:7-8Ni bora kumkimbilia Bwana

kuliko kumtumainia mwanadamu.

9118:9 Za 146:3; Isa 30:2, 3Ni bora kumkimbilia Bwana

kuliko kuwatumainia wakuu.

10118:10 Za 37:9Mataifa yote yalinizunguka,

lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

11118:11 Za 88:17; 3:6Walinizunguka pande zote,

lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

12118:12 Mhu 7:6; Za 58:9; 37:9; Kum 1:44Walinizunguka kama kundi la nyuki,

lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo;

kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

13118:13 Za 118:7; 86:17; 2Nya 18:31Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka,

lakini Bwana alinisaidia.

14118:14 Kut 15:2; Za 62:2Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu,

yeye amefanyika wokovu wangu.

15118:15 Ay 8:21; Lk 1:51; Za 106:5; 89:13; 108:6; Kut 15:6Sauti za shangwe na ushindi

zinavuma hemani mwa wenye haki:

“Mkono wa kuume wa Bwana

umetenda mambo makuu!

16118:16 Kut 15:6Mkono wa kuume wa Bwana

umeinuliwa juu,

mkono wa kuume wa Bwana

umetenda mambo makuu!”

17118:17 Hab 1:12; Za 6:5; 64:9; 71:16; 73:28; Kum 32:3Sitakufa, bali nitaishi,

nami nitatangaza yale Bwana aliyoyatenda.

18118:18 Yer 31:18; Ebr 12:5; 1Kor 11:32; Za 86:13; Mit 3:11, 12Bwana ameniadhibu vikali,

lakini hakuniacha nife.

19118:19 Isa 26:2; Za 24:7; 100:4Nifungulie malango ya haki,

nami nitaingia na kumshukuru Bwana.

20118:20 Ufu 22:14; Za 122:1, 2; 15:1, 2; 24:3-4Hili ni lango la Bwana

ambalo wenye haki wanaweza kuliingia.

21118:21 Za 118:5; 27:1Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu,

umekuwa wokovu wangu.

22118:22 Mdo 4:11; Isa 8:14; 17:10; 19:13; 28:16; Mt 21:42; Lk 20:17; Zek 4:7; 10:4; Mk 12:10; 1Pet 2:7; Efe 2:20Jiwe walilolikataa waashi,

limekuwa jiwe kuu la pembeni.

23118:23 Ay 5:9; Mt 21:42; Mk 12:11Bwana ametenda hili,

nalo ni la kushangaza machoni petu.

24118:24 Za 70:4; 2Kor 6:2Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya,

tushangilie na kufurahi ndani yake.

25118:25 Za 28:9; 116:4Ee Bwana, tuokoe,

Ee Bwana, utujalie mafanikio.

26118:26 Zek 4:7; Mt 11:3; 21:9; 23:39; Mk 11:9; Lk 13:35; 19:38; Yn 12:13; Za 129:8Heri yule ajaye kwa jina la Bwana.

Kutoka nyumba ya Bwana tunakubariki.

27118:27 Za 27:1; Mal 4:2; Isa 60:1; 58:10; 19:20; 1Fal 18:21; 1Pet 2:9; Mik 7:9; Law 23:40; Es 8:2; Kut 27:2Bwana ndiye Mungu,

naye ametuangazia nuru yake.

Mkiwa na matawi mkononi,

unganeni kwenye maandamano ya sikukuu

hadi kwenye pembe za madhabahu.

28118:28 Mwa 28:21; Za 16:2; 63:1; Isa 25:1; Kut 15:2Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru,

wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.

29Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.