Zaburi 115
Mungu Mmoja Wa Kweli
1115:1 Za 29:2; 96:8; Kut 34:6Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi,
bali utukufu ni kwa jina lako,
kwa sababu ya upendo
na uaminifu wako.
2115:2 Za 42:3, 10; 79:10; Yoe 2:17Kwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wao?”
3115:3 Ezr 5:11; Neh 1:4; Za 136:26; 135:6; 103:19; Mit 6:9; Dan 4:35; 1Nya 16:26Mungu wetu yuko mbinguni,
naye hufanya lolote limpendezalo.
4115:4 2Fal 19:18; 2Nya 32:19; Yer 10:3-5; Mdo 19:26; Kum 4:28; Ufu 9:20; Za 135:15, 16; Isa 40:19; Hos 8:6; 1Kor 10:19, 20Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
5115:5 Yer 10:5Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
6zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
zina pua, lakini haziwezi kunusa;
7zina mikono, lakini haziwezi kupapasa,
zina miguu, lakini haziwezi kutembea;
wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
8115:8 Za 135:18; Isa 44:9, 10; Yon 2:8; Hab 2:18Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
9115:9 Za 37:3; 62:8; 33:20; Mit 30:5Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
10115:10 Kut 30:30; Za 118:3; Mal 2:7Ee nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
11115:11 Za 22:23; 103:11; 118:4Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
12115:12 1Nya 16:15; Mwa 12:2; Efe 1:3Bwana anatukumbuka na atatubariki:
ataibariki nyumba ya Israeli,
ataibariki nyumba ya Aroni,
13115:13 Za 24:4; 112:1; Law 26:3; Mit 10:6; Kum 11:27atawabariki wale wanaomcha Bwana,
wadogo kwa wakubwa.
14115:14 Kum 1:11Bwana na awawezeshe kuongezeka,
ninyi na watoto wenu.
15115:15 Mdo 14:15; Ufu 10:6; Za 96:5; Mwa 1:1; 14:19Mbarikiwe na Bwana
Muumba wa mbingu na dunia.
16115:16 Za 89:11; Mwa 1:28; 8:6-8Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana,
lakini dunia amempa mwanadamu.
17115:17 Za 88:10-12Sio wafu wanaomsifu Bwana,
wale washukao mahali pa kimya,115:17 Mahali pa kimya maana yake ni Kuzimu, yaani Sheol kwa Kiebrania.
18115:18 Za 111:1; 113:2; 28:6; 33:2; 105:1; 145:2; Dan 2:20bali ni sisi tunaomtukuza Bwana,
sasa na hata milele.
Msifuni Bwana.115:18 Msifuni Bwana ni Kiebrania Hallelu Yah.