Zaburi 113
Kumsifu Bwana Kwa Wema Wake
1113:1 Za 22:23; 34:22; 103:21; 134:1Msifuni Bwana.
Enyi watumishi wa Bwana msifuni,
lisifuni jina la Bwana.
2113:2 Za 30:4; 48:10; 145:21; 148:13; 149:3; 115:18; 131:3; Isa 12:4; Dan 2:20Jina la Bwana na lisifiwe,
sasa na hata milele.
3113:3 Isa 24:15; 45:6; 59:19; Mal 1:11Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake,
jina la Bwana linapaswa kusifiwa.
4113:4 Za 99:2; 8:1; 57:11Bwana ametukuka juu ya mataifa yote,
utukufu wake juu ya mbingu.
5113:5 Kut 8:10; Ay 16:19; Za 35:10; 103:19Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu,
Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi,
6113:6 Za 11:4; 138:6; Isa 57:15ambaye huinama atazame chini
aone mbingu na nchi?
7113:7 1Sam 2:8; Za 35:10; 68:10; 140:12; 107:41Huwainua maskini kutoka mavumbini,
na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala,
8113:8 2Sam 9:11huwaketisha pamoja na wakuu,
pamoja na wakuu wa watu wake.
9113:9 1Sam 2:5Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake,
akiwa mama watoto mwenye furaha.
Msifuni Bwana.