Zaburi 108 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 108:1-13

Zaburi 108

Kuomba Msaada Dhidi Ya Adui

(Zaburi 57:7-11; 60:5-12)

Wimbo. Zaburi ya Daudi.

1108:1 Za 112:7; 119:30, 112; 18:49Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti;

nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

2108:2 Ay 21:12Amka, kinubi na zeze!

Nitayaamsha mapambazuko.

3Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa;

nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.

4108:4 Hes 14:18; Kum 7:9; Kut 34:6; Za 36:5; Mik 7:18-20Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu;

uaminifu wako unazifikia anga.

5108:5 Za 8:1; 57:5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,

utukufu wako na uenee duniani kote.

6108:6 Ay 40:14Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume,

ili wale uwapendao wapate kuokolewa.

7108:7 Za 89:35; 68:35; 102:19; Mwa 12:6; 33:17Mungu amenena kutoka patakatifu pake:

“Nitaigawa Shekemu kwa ushindi

na kulipima Bonde la Sukothi.

8108:8 Za 78:68; Mwa 49:10Gileadi ni yangu, Manase ni yangu,

Efraimu ni kofia yangu ya chuma,

nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.

9108:9 Mwa 19:37; 2Sam 8:1, 13-14Moabu ni sinia langu la kunawia,

juu ya Edomu natupa kiatu changu;

nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”

10108:10 Za 60:9Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome?

Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?

11108:11 Za 44:9Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi,

na hutoki tena na majeshi yetu?

12108:12 Isa 10:3; 30:3, 5; 31:3; Yer 2:36; 17:7; Za 118:8; 146:3Tuletee msaada dhidi ya adui,

kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.

13108:13 Za 44:5; Isa 22:5; 63:3, 6; 25:10; Mao 1:15; Mal 4:3; Ufu 14:9Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi,

naye atawaponda adui zetu.