Zaburi 107 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 107:1-43

KITABU CHA TANO

(Zaburi 107–150)

Zaburi 107

Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake

1107:1 1Nya 16:8; 2Nya 5:13; 7:3; Mt 19:17Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema,

upendo wake wadumu milele.

2107:2 Za 106:10; Isa 35:9Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi,

wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui,

3107:3 Za 106:47; Isa 49:12; Hes 1:9; Yer 29:14; Eze 39:27wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali,

kutoka mashariki na magharibi,

kutoka kaskazini na kusini.

4107:4 Yos 5:6; Za 107:36Baadhi yao walitangatanga jangwani,

hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi.

5107:5 Kut 16:3; 15:22; 17:2Walikuwa na njaa na kiu,

nafsi zao zikadhoofika.

6107:6 Kut 14:10; Za 50:15; Isa 41:17; Hos 5:15; Yer 29:12-14Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,

naye akawaokoa kutoka taabu yao.

7107:7 Ezr 8:21, 36; Isa 38:12Akawaongoza kwa njia iliyo sawa

hadi mji ambao wangeweza kuishi.

8107:8 Za 105:1; 6:4; 75:1Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,

na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,

9107:9 Za 22:26; 63:5; 23:1; 34:10; Mt 5:6; Yer 31:25; Lk 1:53; Isa 55:1; 58:11kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu,

na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema.

10107:10 Za 107:14; 88:6; 143:3; 102:20; Isa 9:2; 42:7, 16; 49:9; 61:1; Mik 7:9; Ay 36:8Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu,

wafungwa wakiteseka katika minyororo,

11107:11 Za 5:10; Hes 14:11; 1Fal 22:5; 2Nya 36:16kwa sababu walikuwa wameasi

dhidi ya maneno ya Mungu

na kudharau shauri

la Aliye Juu Sana.

12107:12 Isa 63:5; Za 72:12; 2Fal 14:26Aliwatumikisha kwa kazi ngumu;

walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia.

13107:13 Za 106:8Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,

naye akawaokoa kutoka taabu yao.

14107:14 Isa 9:2; 42:7; 59:9; 50:10; 60:2; 29:18; Ay 36:8; Lk 1:79; Za 86:13; 116:16; 146:7; Mdo 12:7Akawatoa katika giza na huzuni kuu

na akavunja minyororo yao.

15107:15 Za 107:8, 21, 31; 105:1; 6:4; 75:1Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,

na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,

16107:16 Isa 45:2kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba

na kukata mapingo ya chuma.

17107:17 Za 53:1; 25:7; Law 14:1; 26:16; Isa 65:6, 7; Yer 30:14, 15; Gal 6:7, 8; Mt 1:22; Mao 3:39Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao,

wakapata mateso kwa sababu ya uovu wao.

18107:18 Ay 3:24; 6:6; 17:16; 33:22Wakachukia kabisa vyakula vyote,

wakakaribia malango ya mauti.

19107:19 Za 107:13; 5:2; 34:4Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,

naye akawaokoa kutoka taabu yao.

20107:20 Kum 32:2; Mt 8:8; 2Fal 20:4; Lk 7:7; Kut 15:26; Hes 21:8; Za 30:3; 16:10; 56:13; 147:15; Ay 33:28Akalituma neno lake na kuwaponya,

akawaokoa kutoka maangamizo yao.

21107:21 Za 107:15; 6:4; 75:1Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,

na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.

22107:22 Law 7:12; Za 9:11; 73:28; 65:8; 50:14; 118:17; Ay 8:21; Ebr 13:15Na watoe dhabihu za kushukuru,

na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha.

23107:23 Isa 42:10; Za 104:26Wengine walisafiri baharini kwa meli,

walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu.

24107:24 Za 64:9; 111:2; 143:5Waliziona kazi za Bwana,

matendo yake ya ajabu kilindini.

25107:25 Za 105:31; 50:3; 93:3Kwa maana alisema na kuamsha tufani

iliyoinua mawimbi juu.

26107:26 Za 22:14; Isa 13:7; Nah 2:10; Lk 8:23; Yos 2:11Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini,

katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka.

27107:27 Isa 19:14; 24:20; 28:7Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi,

ujanja wao ukafikia ukomo.

28107:28 Za 107:19; 4:1; Yon 1:6Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,

naye akawatoa kwenye taabu yao.

29107:29 Lk 8:24; Za 93:3; 65:7; Mk 4:39-41; Yon 1:15; Isa 50:2; Mt 8:26Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono,

mawimbi ya bahari yakatulia.

30107:30 Za 107:7Walifurahi ilipokuwa shwari,

naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani.

31107:31 Za 107:15; 6:4; 75:1; 106:2Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,

na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.

32107:32 Za 30:1; 34:3; 99:5; 1:5; 22:22; 26:12; 35:18Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu,

na wamsifu katika baraza la wazee.

33107:33 1Fal 17:1; Yoe 1:20; Isa 41:15; 42:15; 50:2; 34:9, 10; Eze 30:12; Nah 1:4; Za 74:15; 104:10Yeye aligeuza mito kuwa jangwa,

chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu,

34107:34 Mwa 13:10nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa,

kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo.

35107:35 2Fal 3:17; Za 105:41; 126:4; Isa 43:19; 51:3; 35:7; Ay 38:26Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji,

nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zitiririkazo;

36107:36 Mdo 17:26aliwaleta wenye njaa wakaishi humo,

nao wakajenga mji wangeweza kuishi.

37107:37 2Fal 19:29; Isa 37:30Walilima mashamba na kupanda mizabibu,

nayo ikazaa matunda mengi,

38107:38 Mwa 12:2; 49:25; Kum 7:13Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana,

wala hakuruhusu mifugo yao kupungua.

39107:39 2Fal 10:32; Eze 5:12; Za 44:9Kisha hesabu yao ilipungua, na walinyenyekeshwa

kwa kuonewa, maafa na huzuni.

40107:40 Ay 12:18, 21; Kum 32:10Yeye ambaye huwamwagia dharau wakuu,

aliwafanya watangetange nyikani isiyo na njia.

41107:41 1Sam 2:8; 2Sam 7:8; Za 113:7-9; Ay 21:11; 8:7Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao,

na kuongeza jamaa zao kama makundi ya kondoo.

42107:42 Ay 22:19; 5:16; Mit 10:11; Rum 3:19; Za 97:10-12Wanyofu wataona na kufurahi,

lakini waovu wote watafunga vinywa vyao.

43107:43 Yer 9:12; Hos 14:9; Za 103:11; Dan 12:10Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya,

na atafakari upendo mkuu wa Bwana.