Zaburi 106 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 106:1-48

Zaburi 106

Wema Wa Bwana Kwa Watu Wake

1106:1 Ezr 3:11; Za 63:7; 22:23; 103:2; 119:68; 136:1-26; Yer 33:11; Mt 19:17Msifuni Bwana.

Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

2106:2 Za 40:5; 71:16Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Bwana

au kutangaza kikamilifu sifa zake?

3106:3 Yer 22:15, 16; Mt 22:37; Za 15:2; 112:5; Hos 12:6Heri wale wanaodumisha haki,

ambao daima wanafanya yaliyo mema.

4106:4 Za 25:6-7; 77:7; Mwa 50:24Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako,

uwe msaada wangu unapowaokoa,

5106:5 Kum 30:15; Za 1:3; 105:6; 20:5; 27:5; 47:5; 118:15; Kut 34:9ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako,

niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako,

na kuungana na urithi wako katika kukusifu.

6106:6 1Fal 8:47; Neh 1:7; Dan 9:5; Rum 3:9; 2Nya 30:7; Law 26:40Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda,

tumekosa na tumetenda uovu.

7106:7 Amu 3:7; Za 78:42; Kut 14:11, 12Wakati baba zetu walipokuwa Misri,

hawakuzingatia maajabu yako,

wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako,

bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.

8106:8 Kut 9:16; 14:30-31; Za 80:3; 107:13; 23:3; 143:11; Isa 25:9; Yoe 2:32; Yos 7:9; Yer 14:7, 21Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake,

ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu.

9106:9 Nah 1:4; Isa 50:3; 63:11-14; Kut 14:21; Za 18:15; 78:13Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka,

akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani.

10106:10 Kut 14:30; Za 107:13; 78:42, 53; Isa 35:9; 62:12Aliwaokoa mikononi mwa adui;

kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa.

11106:11 Kut 14:28Maji yaliwafunika adui zao,

hakunusurika hata mmoja.

12106:12 Kut 15:1-21; Za 105:43Ndipo walipoamini ahadi zake,

nao wakaimba sifa zake.

13106:13 Kut 15:24; 16:28; Hes 27:21Lakini mara walisahau aliyowatendea,

wala hawakungojea shauri lake.

14106:14 1Kor 10:9; Kut 17:2; Za 78:40; 68:7Jangwani walitawaliwa na tamaa zao,

walimjaribu Mungu nyikani.

15106:15 Isa 10:16; Hes 11:33; Kut 16:13; Za 78:29Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba,

lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha.

16106:16 Hes 16:1-3Kambini walimwonea wivu Mose,

na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana.

17106:17 Kum 11:6; 15:12; Hes 16:1Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani,

ikawazika Abiramu na kundi lake.

18106:18 Law 10:2Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao,

mwali wa moto uliwateketeza waovu.

19106:19 Kut 32:4; Mdo 7:41Huko Horebu walitengeneza ndama,

na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma.

20106:20 Yer 2:11; Rum 1:23Waliubadilisha Utukufu wao

kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani.

21106:21 Za 78:11; 75:1; Kum 10:21Walimsahau Mungu aliyewaokoa,

aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri,

22106:22 Za 78:51; Kut 3:20; Kum 4:34miujiza katika nchi ya Hamu

na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu.

23106:23 Kut 32:10-14; Hes 11:2; Eze 13:5; 20:13; Kum 9:19Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza:

kama Mose mteule wake,

asingesimama kati yao na Mungu

kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza.

24106:24 Ebr 3:18; Yer 3:19; Hes 14:11, 30, 31; Kum 8:7Kisha waliidharau ile nchi nzuri,

hawakuiamini ahadi yake.

25106:25 Kut 15:24; Kum 1:27; 1Kor 10:10Walinungʼunika ndani ya mahema yao,

wala hawakumtii Bwana.

26106:26 Hes 14:23; Ebr 4:3; 3:17; Kum 2:14Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa

kwamba atawafanya waanguke jangwani,

27106:27 Law 26:33kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa,

na kuwatawanya katika nchi zote.

28106:28 Hes 23:28; 25:2, 3; Kum 4:3; Hos 9:10; Ufu 2:14Walijifunga nira na Baali wa Peori,

wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai.

29106:29 Za 64:2; 141:4; Hes 16:46; 25:3, 8Waliichochea hasira ya Bwana,

wakamkasirisha kwa matendo yao maovu,

nayo tauni ikazuka katikati yao.

30106:30 Kut 6:25; Hes 25:8Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati,

nayo tauni ikazuiliwa.

31106:31 Mwa 15:6; Za 49:11; Hes 15:11-13Hili likahesabiwa kwake haki,

kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo.

32106:32 Kum 1:37; Kut 17:7; Hes 20:2-13Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana,

janga likampata Mose kwa sababu yao;

33106:33 Kut 17:4-7; 23:21; Yak 3:2; Isa 63:10; Za 107:11; 51:11; Hes 20:8-12kwa maana walimwasi Roho wa Mungu,

na maneno yasiyofaa yakatoka midomoni kwa Mose.

34106:34 Amu 1:21, 27-36; 2:2; Yos 9:15; Kum 2:34; 7:2, 16; 20:10; Kut 23:24Hawakuyaangamiza yale mataifa

kama Bwana alivyowaagiza,

35106:35 Amu 3:5, 6; Ezr 9:1, 2bali walijichanganya na mataifa

na wakazikubali desturi zao.

36106:36 Kut 10:7; 23:33; Amu 2:12; 2Fal 17:8-11; 2Nya 33:2-7; Kum 7:10, 16Waliabudu sanamu zao,

zikawa mtego kwao.

37106:37 Isa 57:5; Kut 10:7; 22:20; Law 18:21; Kum 32:17; 12:31; 7:16; 1Kor 10:20; Eze 16:20-21Wakawatoa wana wao

na binti zao dhabihu kwa mashetani.

38106:38 2Fal 3:27; Hes 35:33; Law 18:21; Kum 18:10Walimwaga damu isiyo na hatia,

damu za wana wao na binti zao,

ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani,

nayo nchi ikanajisika kwa damu zao.

39106:39 Mwa 3:17; Law 18:24; Eze 20:18; Hes 15:39Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda;

kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba.

40106:40 Law 26:28; Kut 34:9; 9:29Kwa hiyo Bwana akawakasirikia watu wake

na akauchukia sana urithi wake.

41106:41 Amu 2:14; Neh 9:27Akawakabidhi kwa mataifa

na adui zao wakawatawala.

42106:42 Amu 4:3Adui zao wakawaonea

na kuwatia chini ya mamlaka yao.

43106:43 Amu 7:1-25; 2:16-19; 6:1-7; Yos 10:14; Neh 9:28Mara nyingi aliwaokoa

lakini walikuwa wamezama kwenye uasi,

nao wakajiharibu katika dhambi zao.

44106:44 Amu 3:9; 10:10Lakini akaangalia mateso yao

wakati aliposikia kilio chao;

45106:45 Mwa 9:15; Lk 1:72; Za 105:8; 103:11; 17:7; Law 26:41; Mao 3:32; Kut 32:14kwa ajili yao akakumbuka agano lake,

na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake.

46106:46 1Nya 16:8; Mt 19:17; 2Nya 5:13; 7:3Akawafanya wahurumiwe

na wote waliowashikilia mateka.

47106:47 Za 147:2; 105:1; 30:4; 99:3; 28:9; 107:3; Isa 11:12; 27:13; 56:8; 66:20; Yer 31:8; Lk 1:74; Eze 20:34; Mik 4:6; 2Kor 5:15Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe.

Tukusanye tena kutoka kwa mataifa,

ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu,

na kushangilia katika sifa zako.

48106:48 Za 41:13; 72:19Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli,

tangu milele na hata milele.

Watu wote na waseme, “Amen!”

Msifuni Bwana.