Zaburi 105 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Zaburi 105:1-45

Zaburi 105

Uaminifu Wa Mungu Kwa Israeli

(1 Nyakati 16:8-22)

1105:1 1Nya 16:34; Za 80:18; 99:6; 116:13; Yoe 2:32; Mdo 2:21; Isa 12:4Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,

wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.

2105:2 Za 30:4; 146:2; 33:3; 96:1; 7:17; 18:49; 27:6; 59:17; 71:22; 75:1Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa,

waambieni matendo yake yote ya ajabu.

3105:3 Za 89:16Lishangilieni jina lake takatifu,

mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.

4105:4 Za 24:6; 27:8Mtafuteni Bwana na nguvu zake,

utafuteni uso wake siku zote.

5105:5 Za 40:5; Kum 7:18; 8:2Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,

miujiza yake na hukumu alizozitamka,

6105:6 Za 105:42; Kum 10:15; Za 106:5enyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake,

enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

7105:7 Isa 26:8Yeye ndiye Bwana Mungu wetu,

hukumu zake zimo duniani pote.

8105:8 Mwa 9:15; Za 106:45; 111:5; Eze 16:60; Lk 1:72Hulikumbuka agano lake milele,

neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,

9105:9 Mwa 22:16-18; 15:18; Ebr 6:17; Lk 1:73; 17:2; 12:7; Gal 3:15-18; Dan 9:4agano alilolifanya na Abrahamu,

kiapo alichomwapia Isaki.

10105:10 Mwa 28:13-15; Isa 55:3Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,

kwa Israeli liwe agano la milele:

11105:11 Mwa 12:7; Hes 34:2“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani

kuwa sehemu utakayoirithi.”

12105:12 Kum 7:7; Ebr 11:9; Mwa 17:8; 23:4; 34:30Walipokuwa wachache kwa idadi,

wachache sana na wageni ndani yake,

13105:13 Mwa 15:13-16; Hes 32:13; 33:3-49walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,

kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.

14105:14 Mwa 35:5; 12:17-20; 20:3; Za 9:5Hakuruhusu mtu yeyote awaonee;

kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:

15105:15 Mwa 26:11; 20:7; 1Sam 12:3“Msiwaguse niliowatia mafuta;

msiwadhuru manabii wangu.”

16105:16 Isa 3:1; Law 26:26; Mwa 12:10; 41:54; 2Fal 8:1; Eze 4:16Akaiita njaa juu ya nchi

na kuharibu chakula chao chote,

17105:17 Mwa 45:5; 37:28; Mdo 7:9naye akatuma mtu mbele yao,

Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa.

18105:18 Mwa 40:15Walichubua miguu yake kwa minyororo,

shingo yake ilifungwa kwa chuma,

19105:19 Mwa 12:10; 41:40; 40:20-21hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia,

hadi neno la Bwana lilipomthibitisha.

20105:20 Mwa 41:14Mfalme alituma watu wakamfungua,

mtawala wa watu alimwachia huru.

21Alimfanya mkuu wa nyumba yake,

mtawala juu ya vyote alivyokuwa navyo,

22105:22 Mwa 41:43-44; 41:40kuwaelekeza wakuu wa mfalme apendavyo

na kuwafundisha wazee wake hekima.

23105:23 Mdo 7:15; 13:17; Mwa 46:6; 47:28; Za 78:51Kisha Israeli akaingia Misri,

Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu.

24105:24 Kut 1:7; Kum 26:7; Mdo 7:17Bwana aliwafanya watu wake kuzaana sana,

akawafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao,

25105:25 Kut 4:21; 1:6-10; Mdo 7:19ndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake,

wakatenda hila dhidi ya watumishi wake.

26105:26 Kut 3:10; 4:16; Hes 33:1; 16:5; 17:5-8Akamtuma Mose mtumishi wake,

pamoja na Aroni, aliyemchagua.

27105:27 Za 105:28-37; Kut 7:8; 12:51; 4:17; 10:1; 3:20; Dan 4:3Walifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao,

miujiza yake katika nchi ya Hamu.

28105:28 Mwa 1:4; Za 99:7; Kut 10:22; 7:22Alituma giza na nchi ikajaa giza,

kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake?

29105:29 Za 78:44; Kut 7:21Aligeuza maji yao kuwa damu,

ikasababisha samaki wao kufa.

30105:30 Kut 8:2, 6Nchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia

hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao.

31105:31 Za 78:45; 107:25; 148:8; Kut 8:16-18; 8:21-24Alisema, yakaja makundi ya mainzi,

na viroboto katika nchi yao yote.

32105:32 Kut 9:22-25; Ay 38:22; Za 78:47Alibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe,

yenye umeme wa radi nchini yao yote,

33105:33 Za 78:47; Kut 10:5, 12akaharibu mizabibu yao na miti ya tini,

na akaangamiza miti ya nchi yao.

34105:34 Za 107:25; Kut 10:4, 12-15; 1Fal 8:27; Yoe 1:6Alisema, nzige wakaja,

tunutu wasio na idadi,

35wakala kila jani katika nchi yao,

wakala mazao ya ardhi yao.

36105:36 Kut 4:23; 12:12Kisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao,

matunda ya kwanza ya ujana wao wote.

37105:37 Kut 3:21, 22Akawatoa Israeli katika nchi

wakiwa na fedha na dhahabu nyingi,

wala hakuna hata mmoja

kutoka kabila zao aliyejikwaa.

38105:38 Kut 15:16Misri ilifurahi walipoondoka,

kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia.

39105:39 Kut 13:21; 1Kor 10:1; Za 78:14; Neh 9:12Alitandaza wingu kama kifuniko,

na moto kuwamulikia usiku.

40105:40 Za 78:18; Kut 16:4; Yn 6:31; Kut 16:12Waliomba, naye akawaletea kware,

akawashibisha kwa mkate wa mbinguni.

41105:41 Hes 20:11; 1Kor 10:4; Kut 17:6; Neh 9:15; Isa 48:21Alipasua mwamba, maji yakabubujika,

yakatiririka jangwani kama mto.

42105:42 Mwa 15:1-4, 13-16; 13:14-17Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu,

aliyompa Abrahamu mtumishi wake.

43105:43 Kut 15:1-19; Za 106:12Aliwatoa watu wake kwa furaha,

wateule wake kwa kelele za shangwe,

44105:44 Kum 6:10-11; Za 106:12akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi

wa mali wengine walikuwa wameitaabikia:

45105:45 Kum 6:14-21; 4:1, 40; Za 105:35; 78:5-7alifanya haya ili wayashike mausia yake

na kuzitii sheria zake.

Msifuni Bwana.105:45 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.